-
ICJ: Marekani ilikiuka sheria ya kimataifa kuzuia mali za Iran, iilipe fidia
Mar 30, 2023 23:18Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ) yenye makao yake mjini The Hague wamehukumu kuwa Marekani ilikiuka sheria za kimataifa kwa kuziruhusu mahakama za nchi hiyo kutaifisha mali zenye thamani ya takribani dola bilioni mbili kutoka kwa makampuni ya Iran, na kuiamuru Washington ilipe fidia, kiwango ambacho kitafahamika hapo baadaye.
-
China: Luteka ya pamoja na Iran, Russia imeimarisha ushirikiano wa pande tatu
Mar 30, 2023 22:46China imepongeza kufanyika kwa mafanikio hivi karibuni mazoezi ya pamoja ya kijeshi baina ya nchi hiyo, Iran na Russia katika Bahari ya Oman na kueleza kuwa, luteka hiyo imeimarisha ushirikiano na urafiki wa pande tatu katika usalama wa baharini.
-
Alkhamisi, tarehe 30 Machi, 2023
Mar 29, 2023 23:13Leo ni Alkhamisi tarehe 8 Ramadhani 1444 Hijria sawa na 30 Machi 2023.
-
Amir Abdollahian: Mlango wa mazungumzo ya nyuklia hautabakia wazi milele
Mar 28, 2023 03:43Hossein Amir Abdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema rasimu ya mpango wa kuainisha kiwango cha mazungumzo ya nyuklia inajadiliwa katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) na kusisitiza kwamba mlango wa mazungumzo hayo hautabakia wazi milele.
-
Iran yalaani vitendo vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu Denmark
Mar 27, 2023 23:33Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani wimbi la kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu na makundi yenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia nchini Denmark na katika nchi nyingine za Ulaya.
-
Ripoti: Baadhi ya mashirika ajinabi yalihusika na mauaji ya polisi wa Iran
Mar 27, 2023 08:09Baraza Kuu la Haki za Binadamu la Iran (HCHR) limechapisha ripoti mpya iliyofichua nafasi ya nchi za Magharibi na mashirika yao katika mauaji ya askari polisi wa Jamhuri ya Kiislamu wakati wa maandamano ya karibuni yaliyochochewa na mataifa hayo ya kibeberu hapa nchini.
-
Trump atiwa hofu na wasiwasi na muungano wa Iran, Saudia, China na Russia
Mar 26, 2023 03:39Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ameeleza hofu na wasi wasi alionao juu ya muungano unaoweza kuanzishwa kati ya Iran, Saudi Arabia, China na Russia.
-
Kukiri Waziri wa Fedha wa Marekani kuhusu athari ndogo za vikwazo dhidi ya Iran
Mar 25, 2023 22:51Janet Yellen Waziri wa Fedha wa Marekani amekiri kuwa vikwazo vya Washington dhidi ya Iran vimekuwa na taathira ndogo kuliko ilivyopangwa."
-
Iran na Oman zajadili kuondolewa vikwazo Tehran
Mar 25, 2023 03:53Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian amezungumza na mwenzake wa Oman, Badr Albusaidi kwa njia ya simu, na wawili hao wamejadili kuhusu hali ya sasa ya mazungumzo ya kuiondolea Jamhuri ya Kiislamu vikwazo vya kidhalimu.
-
Maafisa wa Iran, Lebanon wazungumzia matukio ya kieneo mjini Beirut
Mar 24, 2023 04:21Mkuu wa Baraza la Kistratijia la Mahusiano ya Kigeni la Iran, Kamal Kharrazi amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah mjini Beirut, ambapo wamejadili matukio ya hivi sasa ya kisiasa na kiusalama katika eneo la Asia Magharibi.