Rais wa Iran awashambulia Wamagharibi kwa kutetea vitendo vichafu vya ushoga
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i99858
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyashambulia madola ya Maagharibi kutokana na hatua yao ya kutetea vitendo vichafu vya ushoga na mahusiano ya kingono ya watu wa jinsia moja.
(last modified 2025-07-12T14:05:52+00:00 )
Jul 13, 2023 09:40 UTC

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyashambulia madola ya Maagharibi kutokana na hatua yao ya kutetea vitendo vichafu vya ushoga na mahusiano ya kingono ya watu wa jinsia moja.

Rais Rais Ebrahim Raisi alisema hayo kabla ya kukamilisha safari yake nchini Uganda na kuelekea Zimbabwe ambapo alisisitiza kwamba, madola ya Magharibi yamekuwa yakihujumu misingi ya familia kutokana na kupigia debe uchafu wa mahusiano ya kingono ya watu wa jinsia moja.

Rais wa Iran amekosa vikali tabia ya madola ya Magharibi ya kutumia suala la haki za binadamu kwa ajili ya kushinikiza mataifa huru kama ambavyo ameyakosoa kwa hatua yao ya wa kueneza vitendo vya ushoga, misimamo ya kufurutu ada na ugaidi.

Kadhalika Rais Ibrahim Rais sambamba na kuashiria kwamba, hatua hiyo inalenga kusambaratisha kizazi cha mwanadamu amesifu misimamo ya Uganda kuhusiana na suala hilo.

 

Ibrahim Rais amepongeza pia misimamo ya Iran na Uganda iliyo dhidi ya misimamo ya kufurtu ada na ugaidi na kueleza kwamba, nukta ya ushirikiano baina ya Kampala na Tehran ni utambulisho wao ulio dhidi ya ukoloni.

Kabla ya kukamilisha safari yake nchini Uganda na kuelekea Zimbabwe, akiwa mjini Kampala, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa dini mbalimbali nchini Uganda akiwemo Mufti Mkuu wa nchi hiyo Shekhe Shaaban Ramadhan Mubaje.