-
Baqaei: Njia ya mawasiliano iko wazi kati ya Iran na Marekani ili kubadilishana jumbe
Jan 13, 2026 00:10Esmail Baqaei Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa njia ya mawasiliano iko wazi kati ya Abbas Aragchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Steve Witkoff Mjumbe Maalumu wa Marekani ili kubadilishana jumbe kila inapohitajika.
-
Uingiliaji kati wa Marekani nchini Iran; mfano wazi wa kuyumbisha usalama na kuhimiza vurugu
Jan 12, 2026 09:21Iran imeeleza malalamiko yake makali dhidi ya kauli za Marekani za uingiliaji kati katika barua yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Iran yatangaza siku tatu za kuwaomboleza waliouawa shahidi katika jinai zilizochochewa na US na Israel
Jan 12, 2026 03:09Serikali ya Iran imetangaza siku tatu za maombolezo kwa ajili ya kuwakumbuka waathiriwa, wakiwemo askari wa vikosi vya usalama na wa jeshi la kujitolea, ambao wameuliwa shahidi na wafanyaji fujo na vurugu wanaoungwa mkono na Marekani na utawala wa kizayuni wa Israel, waliojaribu kuteka nyara maandamano ya amani ya wananchi ya kulalamikia hali ya uchumi nchini.
-
Araghchi: Kuna ushahidi unaowahusisha magaidi wa Mossad na vurugu za mauaji zilizofanywa Iran
Jan 12, 2026 03:09Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Abbas Araghchi amesema, kuna ushahidi wa wazi unaohusisha vurugu za mauaji zilizofanywa hapa nchini na magaidi wenye mfungamano na shirika la ujasusi la utawala wa kizayuni wa Israel, Mossad.
-
Pezeshkian: Waliofanya fujo na machafuko Iran si wananchi; ni magaidi kutoka nje
Jan 11, 2026 23:45Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, adui amewaingiza Iran magaidi waliopewa mafunzo maalumu ya kigaidi ili kufanikisha malengo yake na kwamba waliofanya fujo, machafuko na uharibifu katika kona mbalimbali za Iran, si katika wananchi waliokuwa wanaandamana.
-
Waziri Araghchi aanika nafasi ya Marekani, Israel katika ghasia za Iran
Jan 11, 2026 03:25Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi amezionya vikali Marekani na utawala haramu wa Israel juu ya matokeo mabaya ya uchochezi na uungaji mkono wao kwa wafanya fujo na wazua rabsha hapa nchini, akisisitiza kuwa Washington na Tel Aviv zinataka kuyageuza maandamano ya kiuchumi ya wananchi wa Iran kuwa machafuko na ghasia.
-
Wairani kufanya maandamano kote nchini kupinga ghasia na fujo
Jan 11, 2026 03:06Baraza la Uratibu wa Uenezi wa Kiislamu la Iran limetangaza kuwa, wananchi Waislamu wa Jamhuri ya Kiislamu kesho Jumatatu watafanya maandamano katika pembe zote za nchi kulaani ghasia na fujo zilizochochewa hapa nchini na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Marekani inahusika katika kugeuza maandamano ya amani kuwa machafuko nchini Iran
Jan 10, 2026 05:52Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Bw. Amir-Saeid Iravani katika Umoja wa Mataifa ameliandikia barua Baraza la Usalama la umoja huo akisema Marekani imeyageuza malalamiko na maandamano ya amani ya wananchi wa Iran kuwa ghasia na machafuko.
-
Araqchi: Teknolojia haiwezi kuangamizwa kupitia mashambulizi
Jan 10, 2026 00:55Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria mashambulizi ya utawala wa Kizayuni na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran vinavyofanya kazi kwa malengo ya kiraia katika vita vya siku 12 na kusema baadhi ya majengo, taasisi na suhula za nyuklia zinazotumika kwa malengo ya amani za Iran zilidhurika hata hivyo teknolojia haiweza kuangamizwa kupitia mashambulizi.
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa: Waandamanaji watajitenga na wachache wanaovuruga amani
Jan 09, 2026 09:40Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo ya mjini Tehran, Hujjatul Islam Sayyid Mohammad Hassan Abu Torabi Fard amesema, waandamanaji waelewa na wenye ghera ya uhuru na mamlaka imara ya nchi watatenganisha njia yao na ya wachache wanaoitakia mabaya nchi, wafanyao vitendo vya ukatili na kuvuruga nidhamu ya jamii; na hilo ni jambo lenye ulazima usioweza kuepukika.