-
Naibu Waziri wa Ulinzi wa Iran: Tumeunda makombora ya kisasa kulingana na vitisho vya adui
Aug 17, 2018 10:46Naibu Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema, zimeundwa zana, makombora na mifumo ya kiulinzi ya kisasa nchini kulingana na vitisho vya adui na akasisitiza kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katu haianzishi vita lakini ina uwezo mzuri sana wa kujihami na yeyote atakayeichokoza atajuta.
-
Zarif: Marekani imejitakia yenyewe kutengwa kimataifa baada ya kujitoa katika JCPOA
Aug 16, 2018 03:08Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Marekani imejitakia yenyewe kutengwa kimataifa baada ya kujitoa kinyume cha sheria katika mapatano ya nyuklia na Iran.
-
China: Hatutasalimu amri mbele ya mashinikizo ya Marekani kuihusu Iran
Aug 14, 2018 10:31Mkuu wa Shirikisho la Sekta ya Mafuta na Bidhaa za Kemikali nchini China amesema kuwa, Beijing haina nia ya kusalimu amri mbele ya mashinikizo ya Marekani kwa ajili ya kutekeleza vikwazo vya upande mmoja vya Washington dhidi ya Iran.
-
Wakristo wa Iran wamwambia Pompeo: Wafuasi wa dini za wachache Iran hawahitajii usimamizi wa Marekani
Aug 12, 2018 22:21Jumuiya ya Wakristo wa Assyrian nchini Iran imejibu ujumbe wa Twitter wa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani aliyedai kuwa wafuasi wa dini za waliowachache wanasumbuliwa na kunyimwa haki zao za binadamu hapa nchini kwa kusema kuwa: Wafuasi wa dini za waliowachache nchini Iran hawahitaji usimamizi wa Marekani.
-
Rouhani na Putin wabadilishana mawazo kuhusu masuala ya kikanda na kimataifa
Aug 12, 2018 09:07Marais wa Iran na Russia wamejadili na kubadilishana mawazo kuhusu masuala ya pande mbili, ya kikanda na kimataifa katika mazungumzo yao yaliyofanyika leo kandokando ya mkutano wa 5 wa viongozi wa nchi za pwani mwa Bahari ya Kaspi unaofanyika nchini Kazakshtan.
-
Indhari ya Shirika la Kimataifa la Nishati kuhusu kuiwekea vikwazo vya mafuta Iran
Aug 12, 2018 02:45Rais Donald Trump wa Marekani tarehe Nane Mei mwaka huu alikariri madai yasiyo na msingi dhidi ya Iran na kutangaza kujitoa Marekani katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kuvirejesha vikwazo vya nyuklia katika muda wa miezi mitatu hadi sita ijayo. Duru ya kwanza ya vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran imeanza kutekelezwa tangu tarehe 7 mwezi huu wa Agosti; hatua iliyolaaniwa vikali kimataifa.
-
Kiwango cha usafirishaji bidhaa za Iran Kenya chaongezeka
Aug 12, 2018 01:58Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Kenya amesema kiwango cha bidhaa za Iran zinazosafirishwa kupelekwa nchini humo kimeongezeka.
-
Zarif: Hakuna mazungumzo baina ya Iran na Marekani, mkutano wa New York
Aug 11, 2018 22:05Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekanusha ripoti za vyombo vya habari kuhusu uwezekano wa kufanyika mazungumzo baina ya maafisa wa Iran na Marekani kandokando ya mkutano ujao wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.
-
Marekani imebakia kuangalia kwa macho tu uwezo wa kijeshi wa Iran Ghuba ya Uajemi
Aug 09, 2018 09:10Kamanda wa Komandi Kuu wa Jeshi la Marekani amezungumzia luteka mazoezi ya kijeshi yaliyoifanywa hivi karibuni na Jeshi la Majini la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Ghuba ya Uajemi na Lango Bahari la Hormoz na kukiri uwezo mkubwa wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Sharti la Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani kwa ajili ya kuzungumza na Iran bila ya masharti
Aug 08, 2018 02:54Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani ameainisha sharti kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Iran licha ya ombi la Rais Trump la kutaka kufanya mazungumzo na Iran bila ya masharti yoyote.