Kiwango cha usafirishaji bidhaa za Iran Kenya chaongezeka
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i47389-kiwango_cha_usafirishaji_bidhaa_za_iran_kenya_chaongezeka
Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Kenya amesema kiwango cha bidhaa za Iran zinazosafirishwa kupelekwa nchini humo kimeongezeka.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 12, 2018 01:58 UTC
  • Kiwango cha usafirishaji bidhaa za Iran Kenya chaongezeka

Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Kenya amesema kiwango cha bidhaa za Iran zinazosafirishwa kupelekwa nchini humo kimeongezeka.

Hadi Farajvand ameyasema hayo katika kikao na wadau wa sekta ya uchumi wa mkoa wa Qazvin ulioko magharibi mwa Tehran. Amebainisha kuwa tokea mwezi Machi mwaka huu hadi sasa, bidhaa zenye thamani ya dola milioni 79 zimesafirishwa kuelekea nchini Kenya.

Kwa mujibu wa balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Nairobi, marumaru, vyombo vya ufinyazi, mafuta ghafi ya kupikia, makaroni na mazulia ya nyuzi ndizo bidhaa za Iran zilizosafirishwa kwa wingi zaidi kuelekea nchini Kenya katika kipindi hicho.

Katika kikao hicho, Ali Purzahmat, mkuu wa shirika la viwanda, madini na biashara la mkoa wa Qazvin amesema kiwango cha usafirishaji bidhaa za mkoa huo kuelekea nje ya nchi katika mwaka uliopita wa 2017 kilikuwa dola milioni 850 na akaongeza kuwa katika miezi minne iliyopita pia bidhaa zinazozalishwa mkoani humo zenye thamani ya dola milioni 220 zimesafirishwa kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi.

Kenya ni moja ya masoko muhimu ya bidhaa za Iran zinazosafirishwa nje ya nchi, ambapo katika mwaka uliopita wa 2017 huduma na bidhaa zenye thamani ya dola milioni 200 zilisafirishwa kutoka Iran kuelekea nchini humo.

Tangu miaka kadhaa nyuma Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikilipa kipaumbele suala la kustawisha uhusiano wake na nchi za Afrika.../