Pezeshkian: Tutalinda kila inchi ya ardhi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i139898-pezeshkian_tutalinda_kila_inchi_ya_ardhi_ya_iran
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekosoa kauli za maafisa wa Marekani na kusisitiza kwamba Iran italinda ardhi yake yote dhidi ya tishio la aina yoyote.
(last modified 2026-07-15T09:20:04+00:00 )
Jul 15, 2026 09:18 UTC
  • Rais Masoud Pezeshkian
    Rais Masoud Pezeshkian

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekosoa kauli za maafisa wa Marekani na kusisitiza kwamba Iran italinda ardhi yake yote dhidi ya tishio la aina yoyote.

Akijibu matamshi ya Rais wa Marekani, kando ya khitma ya kumkumbuka Kiongozi shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu mjini Tehran, Rais wa Iran Masoud Pezeshkian ameyataja matamshi ya Donald Trump kuwa "ni otuvu wa adabu" na akasema kwamba matamshi kama hayo yanalandana na wazungumzaji wake na hayastahili majibu kutoka Iran.

Donald Trump, katika mahojiano na Fox News alijigamba kwa kufanya uhalifu wa kiivita kwamba ameshambulia miundombinu ya kiraia nchini iran na kudai kwamba: "Tutawapiga vikali sana usiku wa leo, na kisha, wiki ijayo, mambo yatakuwa mabaya sana kwao. Kwa sababu wiki ijayo, tutapiga mitambo ya umeme na madaraja."

Masoud Pezeshkian amesema: "Ni kawaida kuona adui akiendelea kutoa bwabwaja kama hizi, lakini je, ameweza kutimiza malengo yake nyanjani?"

Amehoji kwa kusema: "Wale waliokuwa na nia ya kuirarua na kuikata vipande vipande Iran yetu wako wapi?" na kuongeza: "Tunaamini kwamba lazima tulinde kila inchi ya ardhi yetu kwa vitendo, na matamshi haya yasiyo na adabu yanaoawa na wao wenyewe, sio taifa la Iran."

Akisisitiza kwamba katika hali ya sasa, kuna ulazima wa kudumisha umoja na mshikamano wa ndani, Rais Pezeshkian amesema: "Mwenendo au kitendo chochote kinachoibua mgawanyiko katika jamii kitapunguza nguvu zetu."