-
Iran yaipongeza Afrika Kusini kwa kuwaunga mkono wananchi wa Palestina
Apr 15, 2022 07:39Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameipongeza Afrika Kusini kwa misimamo yake ya kuwaunga mkono na kuwatetea wananchi madhulumu wa Palestina.
-
Tanzania yakaribisha pendekezo la Iran la kutoa elimu na mafunzo ya ujuzi kwa wanawake wa nchi hiyo
Mar 20, 2022 06:27Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu wa Tanzania amekaribisha pendekezo lililotolewa na Makamu wa Rais wa Iran katika Masuala ya Wanawake na Familia la kuwapatia mafunzo ya ujuzi wanawake na wasichana wa Tanzania.
-
Iran yapinga kutumiwa vibaya haki za binadamu kwa malengo ya kibeberu
Mar 03, 2022 09:22Naibu wa Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya kimataifa ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya Haki za Binadamu ya Iran amesema kuwa, Tehran inapinga vikali kutumiwa vibaya suala la haki za binadamu.
-
Iran: Tuko tayari kustawisha uhusiano wetu na nchi za Afrika katika nyuga tofauti
Feb 23, 2022 03:43Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran iko tayari kuimarisha na kustawisha uhusiano wake katika nyuga mbalimbali na nchi za Afrika kama vile kupeleka barani humo uzoefu wake wa kiufundi na kihandisi.
-
Raisi atoa mwito wa kustawishwa uhusiano wa Iran na Msumbiji
Feb 22, 2022 23:21Rais Ebrahim Raisi wa Iran ametoa mwito wa kuboreshwa uhusiano wa pande mbili baina ya Jamhuri ya Kiislamu na Msumbiji katika nyuga tofauti.
-
Amir-Abdollahian afanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali hapa Tehran
Feb 13, 2022 08:59Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kufanya mazungumzo hapa Tehran leo Jumapili na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali aliyeko ziarani hapa nchini.
-
Rais wa Senegal alipongeza taifa la Iran kwa maadhimisho ya Siku ya Mapinduzi ya Kiislamu
Feb 12, 2022 03:25Rais wa Senegal ametoa mkono wa baraka na fanaka kwa serikali na taifa la Iran kwa mnasaba wa kuadhimisha mwaka wa 43 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Sheikh Ibrahim Zakzaky: Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni ya Waislamu wote ulimwenguni
Feb 07, 2022 09:21Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran hayaishii tu katika mipaka ya Iran na wananchi wa taifa hili bali ni mali ya Waislamu wote ulimwenguni.
-
Rais Ebrahim Raisi: Uhusiano wa Iran na nchi za Afrika utaimarishwa zaidi
Jan 24, 2022 10:36Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika kikao chake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Togo kuwa: Suala la kuimarishwa uhusiano wa Iran na nchi za bara la Afrika litafuatiliwa kwa umakini na nguvu zaidi.
-
Kenya yakaribisha wawekezaji kutoka Iran katika sekta za mafuta, dawa na vifaa vya tiba
Jan 20, 2022 23:48Mwambata wa kiuchumi katika ubalozi wa Kenya mjini Tehran amesema nchi yake inakaribisha wawekezaji kutoka Iran kwenda kuwekeza vitega uchumi katika nchi hiyo.