-
Netanyahu apongeza juhudi za Imarati za kuimarisha uhusiano na Israel
Dec 22, 2019 10:33Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel amepongeza jitihada zinazofanywa na Umoja wa Falme za Kiarabu za kutaka kuimarisha na kufanya wa kawaida uhusiano wa utawala huo pandikizi na baadhi ya nchi za Kiarabu.
-
Uamuzi wa Mahakama ya ICC wa kufuatilia jinai za utawala wa Kizayuni
Dec 21, 2019 21:43Hatua zilizo dhidi ya ubinadamu na za ukiukaji sheria zinazochukuliwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina zimekuwa zikilaaniwa mara kwa mara na taasisi za kutetea haki za binadamu na pia za kimataifa. Kutokana na kushtadi kwa hatua hizo za utendaji jinai, taasisi ya kimataifa yenye jukumu la kushughulikia jinai za kivita hivi sasa imepanga kuchunguza suala hilo.
-
Arab League yailaani Brazil kwa kufungua ofisi ya kibiashara Quds tukufu
Dec 20, 2019 08:12Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imeikosoa vikali Brazil kwa kufungua ofisi ya kibiashara katika mji wa Quds huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.
-
Nasrullah: Hizbullah ni tishio kubwa kwa njama za Marekani na Israel
Dec 14, 2019 03:55Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema njama ghalati za Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo zimekuwa zikigonga mwamba kutokana na uwepo na kusimama kidete harakati hiyo ya muqawama.
-
Israel yawakamata viongozi kadhaa wa HAMAS al-Khalil
Dec 12, 2019 21:13Vikosi vya usalama vya utawala haramu wa Israel vimeendeleza chokochoko zake kwa kuwatia mbaroni viongozi kadhaa wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) mjini al-Khalil (Hebron), katika Ukiongo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Azimio la Kongresi ya Marekani dhidi ya uvamizi wa utawala wa Kizayuni katika eneo la Ukingo wa Magharibi
Dec 08, 2019 23:11Serikali ya rais Donald Trump imekuwa ikitekeleza hatua zisizo za kawaida katika uwanja wa kuunga mkono vitendo vilivyo kinyume cha sheria vya utawala haramu wa Israel dhidi ya taifa la Palestina.
-
Israel inawapa mafunzo ya kijeshi wapiganaji wa Haftar Libya
Dec 08, 2019 08:27Gazeti la Qatar la Al-Araby Al-Jadeed limefichua kuwa, jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel linawapa mafunzo ya kijeshi wanamgamboa wa kundi la wapiganaji linaloongozwa na jenerali muasi Khalifa Haftar ambalo linajiita Jeshi la Taifa la Libya.
-
Nukta tano kuhusu jaribio la kombora la utawala wa Kizayuni wa Israel
Dec 08, 2019 03:56Msemaji wa Jeshi la Utawala wa Kizayuni wa Israel tarehe 6 Disemba alitangaza kuwa jeshi la utawala huo lilifanyia jaribio kombora moja katika eneo la Ashdod.
-
UN: Ukaliaji ardhi kwa mabavu wa Israel unaisababishia Palestina hasara ya dola bilioni 2.5 kwa mwaka
Dec 03, 2019 04:17Umoja wa Mataifa umesema hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina inausababishia uchumi wa Wapalestina hasara ya dola bilioni 2.5 kila mwaka.
-
Jamii ya kimataifa yakosolewa kwa kunyamazia kimya jinai za Israel dhidi ya Wapalestina
Dec 02, 2019 08:56Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Palestina imekikosoa vikali kimya cha jamii ya kimataifa mbele ya jinai za utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Wapalestina na kueleza kuwa hilo ni doa baya katika paji la uso la walimwengu.