-
Askari wa Israel aliyekuwa vitani Ghaza na Lebanon ajiua ndani ya gari lake
Jul 07, 2025 15:34Tovuti ya Kiebrania ya Walla imeripoti kuwa, mwanajeshi wa utawala wa Kizayuni Israel, Daniel Edri, amejiua kwa kujichoma moto ndani ya gari lake kwenye msitu karibu na eneo la Safed, kutokana na msongo mkali wa mawazo baada ya kuhudumu kwenye vita vya kinyama vya utawala huo dhidi ya Ghaza na Lebanon.
-
Jenerali Shekarchi: Iran itatoa jibu la kuponda zaidi iwapo Israel itaishambulia tena
Jul 07, 2025 08:02Kamanda mwandamizi wa Jeshi la Iran ameonya kuwa, Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu viko tayari kufanya mashambulizi yenye nguvu na ya maangamizi zaidi dhidi ya vitendo vyovyote vya kichokozi vitakavyofanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya taifa hili.
-
Hamas yakaribisha mwito wa BRICS wa kuondoka vikosi vya Israel huko Palestina
Jul 07, 2025 07:20Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas imekaribisha kwa mikono miwili wito wa kundi la nchi zinazoinukia kiuchumi BRICS kwa utawala haramu wa Israel, wa kukomesha vita vyake vya mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza, na kuondokaa kikamilifu katika eneo hilo la pwani lililozingirwa, na ardhi zote za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.
-
Iran: Ugaidi wa kijeshi wa Israel ni pigo kwa diplomasia, NPT
Jul 06, 2025 14:48Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi amelaani uvamizi na hujuma zilizofanywa hivi karibuni na Marekani na Israel dhidi ya Iran, na kuzieleza kuwa pigo kubwa kwa diplomasia, utawala wa sheria na Mkataba wa Kuzuia Uzalishaji na Uenezaji wa Silaha za Nyuklia (NPT).
-
Sababu za Marekani na Israel kuwapiga risasi Wapalestina kwenye safu za misaada huko Gaza
Jul 05, 2025 22:55Wakandarasi wa usalama wa Marekani wanatumia risasi za moto, maguruneti, na gesi ya kuwasha dhidi ya raia katika vituo vya usambazaji wa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza.
-
Kwa nini Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kuwekewa vikwazo vya silaha Israel?
Jul 05, 2025 11:50Francesca Albanese, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ameitaja hali ya Gaza kuwa ni "mojawapo ya mauaji ya kikatili zaidi katika historia ya sasa" na kutoa wito wa kuwekewa vikwazo vya silaha Israel na kusitishwa uhusiano wote wa kibiashara na uwekezaji na utawala huo ghasibu.
-
Kwa nini shambulio la Israel na Marekani dhidi ya Iran limetoa pigo kubwa kwa NPT?
Jul 03, 2025 03:56Tovuti ya Kiingereza ya Al Jazeera imezungumzia matokeo ya hujuma za karibuni za Marekani na Wazayuni katika ardhi ya Iran na vituo vyake vya nyuklia, na kuandika kwamba vita vya siku 12 havijafanikiwa chochote isipokuwa kuharibu uaminifu wa kiwango fulani uliokuwepo kuhusiana na Mkataba wa Kuzuia Usambazaji wa Nyuklia (NPT).
-
Katibu Mkuu wa Hizbullah: Iran ndiye mshindi wa Vita vya Siku 12
Jun 28, 2025 02:49Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema, Iran ndiye mshindi wa makabiliano baina yake na adui mzayuni.
-
Watumiaji wa kigeni wa mitandao ya kijamii: Grossi ni kikaragosi cha Mossad dhidi ya Iran
Jun 28, 2025 02:44Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) Rafael Grossi ameshambuliwa vikali na watumiaji wa kigeni wa mitandao ya kijamii kwa kushirikiana na Marekani na utawala haramu wa Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hasa baada ya kutaka kuruhusiwa maafisa wa shirika hilo kuingia Iran na kukagua miradi ya nishati ya nyuklia iliyoshambuliwa na Marekani.
-
Ben-Gvir awaruhusu walowezi wa Kizayuni kuimba na kudansi kwenye Msikiti wa Al-Aqsa
Jun 28, 2025 02:22Waziri maluuni wa mambo ya ndani wa utawala wa Kizayuni wa Israel Itamar Ben-Gvir ametoa ruhusa kwa walowezi haramu wa Kizayuni kuimba na kudansi kwenye eneo la Msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa Baitul-Muqaddas unaokaliwa kwa mabavu.