-
Iran yalaani mwenendo wa madola makubwa wa kuitunukia Israel 'haki maalumu' ya kufanyia uchokozi
Dec 12, 2025 11:03Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, sera za mataifa makubwa katika Asia Magharibi zimetengeneza "haki maalumu kwa ajili ya utawala wa Kizayuni," hali ambayo imeiwezesha Israel kufanya uchokozi wa kijeshi katika eneo zima, ikiwa ni pamoja na dhidi ya Iran, bila kukabiliwa na mjibizo wa maana kimataifa kwa uchokozi wake huo.
-
Ripoti: US inaishinikiza Israel iuondoe mlima wa kifusi uliozagaa Ghaza baada ya miaka 2 ya vita
Dec 12, 2025 10:10Marekani imeitaka Israel ibebe jukumu la kuondoa vifusi vikubwa vilivyotapakaa kwenye kila pembe ya Ukanda wa Ghaza baada ya zaidi ya miaka miwili ya vita vya kinyama na mauaji ya kimbari iliyofanya dhidi ya Wapalestina wa eneo hilo, pamoja na uharibifu mkubwa uliosababishwa na mashambulizi yake ya anga na matingatinga ya kivita. Hayo yameelezwa na toleo la Alkhamisi la gazeti la kizayuni la Yedioth Ahronoth.
-
Ghana yajibu mapigo kwa Israel, yawatimua wazayuni watatu waliowasili nchini humo
Dec 11, 2025 06:10Serikali ya Ghana imewatimua kwa kuwarejesha walikotoka Waisraeli watatu, katika hatua ya kujibu mapigo na kulipiza kisasi dhidi ya utawala wa kizayuni wa Israel baada ya hapo awali kulalamikia kunyanywaswa raia wake katika uwanja wa ndege wa Ben Gurion, mjini Tel Aviv.
-
Ghana yakosoa vitendo vya kinyama vya Israel dhidi ya raia wa nchi hiyo waliokwenda mkutanoni Tel Aviv
Dec 11, 2025 03:35Ghana jana Jumatano kile ilikosoa kile ilichokitaja kuwa vitendo vya "kinyama" walivyotendewa raia wa nchi hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) baada ya wasafiri kadhaa wa Ghana kuzuiliwa au kufukuzwa .
-
Mwanadiplomasia: Iran iliitia Israel hasara 'kubwa na iliyoenea' wakati wa Vita vya Siku 12
Dec 09, 2025 03:32Mwanadiplomasia mwandamizi wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu iliusababishia utawala wa kizayuni wa Israel uharibifu 'mkubwa na ulioenea' wakati wa uvamizi wake uliofanya mwezi Juni dhidi ya Iran kwa uungaji mkono wa Marekani.
-
Netanyahu: Israel haitaondoka katika maeneo ya kusini ya Syria iliyoyavamia
Dec 08, 2025 06:30Waziri Mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu amesema, jeshi la utawala huo halitaondoka katika maeneo liliyoyavamia na kuyakalia kwa mabavu ya kusini mwa Syria.
-
Iran: Mkakati mpya wa Usalama wa Taifa wa Marekani unaandikwa hasa kwa ajili ya Israel
Dec 08, 2025 03:07Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Mkakati mpya wa Usalama wa Taifa wa Marekani (NSS) unaobainisha misingi na vipaumbele vya Washington katika sera za nje kimsingi ni hati ya usalama kwa ajili ya utawala wa kizayuni wa Israel.
-
HAMAS: Tuko tayari kukabidhi silaha kwa utawala wa Wapalestina ikiwa Israel itaondoka kikamilifu Ghaza
Dec 08, 2025 02:34Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema, iko tayari kukabidhi silaha zake katika Ukanda wa Ghaza kwa mamlaka ya utawala ya Wapalestina itakayosimamia uendeshaji wa eneo hilo, kwa sharti kwamba uvamizi na ukaliaji ardhi kwa mabavu wa jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel ukomeshwe kikamilifu.
-
Hamas: Mwisho wa Abu Shabab ndio hatima isiyoepukika ya kila msaliti
Dec 05, 2025 10:50Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeonya kwamba mauaji ya mshirika wa Israel na kiongozi wa genge lenye uhusiano na Daesh, Yasser Abu Shabab, ni hatima isiyoepukika ya kila mtu anayechagua kulisaliti taifa na nchi yake na kushirikiana na utawala ghasibu wa Israel.
-
Yasser Abu Shabab, mshirika wa Israel na msaliti wa Wapalestina wa Ghaza aripotiwa kuuawa
Dec 05, 2025 06:55Yasser Abu Shabab, mshirika wa kijeshi wa utawala wa kizayuni wa Israel mwenye uhusiano pia na kundi la kigaidi la DAESH (ISIS), maarufu kwa kuongoza uporaji wa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Ghaza na kwa kuwalenga kwa kuwaua raia wa Palestina, ameripotiwa kuuawa katika eneo hilo.