-
CPJ: Israel ndiyo iliyoua wanahabari wengine zaidi duniani 2025
Feb 26, 2026 01:54Utawala haramu wa Israel uliwaua wanahabari wasiopungua 84 mwaka wa 2025 - idadi kubwa zaidi kuliko dola lolote duniani katika mwaka uliokuwa mbaya zaidi kuwahi kurekodiwa kwa vyombo vya habari.
-
Intelijinsia ya Israel: Jeshi la Marekani linaweza kumudu mashambulizi dhidi ya Iran kwa siku kadhaa tu
Feb 25, 2026 05:35Maafisa wa ujasusi wa Israel wanakadiria kuwa Marekani inaweza kuendeleza mashambulio ya kijeshi kwa "siku nne hadi tano" pekee dhidi ya Iran ikiwa itaanzisha mashambulizi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu. Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya.
-
Ripoti: Israel iliwamiminia risasi, kuwaua wafanyakazi wa misaada Tel al Sultan, Gaza
Feb 24, 2026 22:56Karibu risasi elfu moja zilifyatuliwa na wanajeshi wa Israel katika mauaji ya kiholela dhidi ya wafanyakazi wa misaada huko Tel al-Sultan, Gaza, huku baadhi yao wakiuawa kwa kupigwa risasi kwa karibu, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa hivi karibuni.
-
Israel imepeleka Ghaza maboksi yenye mafuvu na miili iliyonyofolewa ya wanawake Wapalestina
Feb 24, 2026 07:45Mbunge wa kujitegemea, ambaye pia ni kiongozi wa zamani wa chama cha Leba nchini Uingereza Jeremy Corbyn, ametoa simulizi za kutisha zilizotokana na maelezo ya mkurugenzi wa Hospitali ya Al-Shifa katika Ukanda wa Ghaza uliozingirwa, zinazobainisha kwa undani jinsi utawala wa kizayuni wa Israel ulivyopeleka katika eneo hilo masanduku kadhaa yenye mafuvu ya vichwa na mabaki ya Wapalestina yaliyokatwakatwa.
-
Wapalestina wanakoseshwa kufunga na kufungua Saumu kwa wakati kwenye jela za Israel
Feb 24, 2026 00:36Tume moja ya Palestina inayoshughulikia masuala ya Wapalestina wanaoshikiliwa kwenye jela za utawala wa kizayuni wa Israel imezishutumu mamlaka za jela hizo kwa kuwafanya Wapalestina hao washindwe kufunga Saumu zao "kwa wakati sahihi" katika mfungo huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
-
Licha ya vizuizi vikali vya Israel, Wapalestina laki moja wasali I'sha na Tarawehe Masjidul-Aqsa
Feb 21, 2026 07:37Licha ya vizuizi vikali vilivyowekwa na utawala wa Kizayuni wa Israel vya kuingia katika Msikiti wa Al-Aqsa, makumi ya maelfu ya Wapalestina jana usiku walihudhuria katika msikiti huo mtukufu kusali Sala za I'sha na Tarawehe wakati huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
-
Waholanzi 640 waliohudumu katika jeshi la Israel Gaza kushtakiwa?
Feb 19, 2026 23:56Zaidi ya raia 640 wa Uholanzi wamehudumu katika jeshi la Israel wakati wa vita vya mauaji ya halaiki vya utawala huo wa Kizayuni dhidi ya Gaza na kwneye mashambulizi dhidi ya Ukingo wa Magharibi, takwimu mpya zinaonyesha, huku wataalamu wa sheria wakionya kwamba, wale waliohusika wanaweza kushtakiwa chini ya sheria za kimataifa na za nchi hiyo za uhalifu wa kivita.
-
Kwa kuwadia Ramadhani, mlowezi wa kizayuni auchoma moto Msahafu Baitul-Muqaddas
Feb 18, 2026 07:00Mlowezi mmoja Muisraeli wa kizayuni mwenye misimamo ya chuki ameichoma moto nakala ya Kitabu kitakatifu cha Waislamu, Qur'ani, akiwa katika eneo ambalo halijafahamika katika mji wa Baitul-Muqaddas, siku chache kabla ya kuanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
-
Israel yashadidisha mateso kwa Wapalestina inaowashikilia kwenye magereza yake
Feb 17, 2026 23:33Jumuiya ya Wafungwa wa Palestina imetangaza kuwa, kwa mujibu wa ziara za ukaguzi zilizofanywa na wanasheria wake na ushuhuda uliorekodiwa, utawala wa kizayuni wa Israel umeshadidisha udhalilishaji na ushinikizaji wa kimfumo dhidi ya wafungwa Wapalestina unaowashikilia katika magereza yake ya kuogofya.
-
Wakenya: Mradi wa kilimo wa Israel Nakuru ni mwanzo wa unyakuzi wa ardhi zetu
Feb 17, 2026 02:52Mradi wa Israel wa kilimo na makazi wa ekari 520 huko Solai, Kaunti ya Nakuru nchini Kenya umezua mjadala mkali wa kitaifa. Wakenya wametumia mitandao ya kijamii kupinga mradi huo, wanaotaja kuwa mwanzo wa unyakuzi wa ardhi za nchi hiyo na utawala ghasibu wa Israel.