-
Wakenya: Mradi wa kilimo wa Israel Nakuru ni mwanzo wa unyakuzi wa ardhi zetu
Feb 17, 2026 02:52Mradi wa Israel wa kilimo na makazi wa ekari 520 huko Solai, Kaunti ya Nakuru nchini Kenya umezua mjadala mkali wa kitaifa. Wakenya wametumia mitandao ya kijamii kupinga mradi huo, wanaotaja kuwa mwanzo wa unyakuzi wa ardhi za nchi hiyo na utawala ghasibu wa Israel.
-
"Ni muhali kufikia amani na Israel madhali inakiuka haki za Wapalestina"
Feb 16, 2026 06:47Waziri wa Mambo ya Nje na Wahamiaji wa Palestina, Varsen Aghabekian Shahin amesema kufikia amani na Israel "haiyumkiniki" madhali haki za Wapalestina zinakiukwa na utawala huo wa Kizayuni, akisisitiza kwamba sheria za kimataifa zinapasa kuzingatiwa, na uchukuaji wa hatua za upande mmoja lazima ukomeshwe.
-
Je, China ina msimamo gani kuhusu hatua mpya za utawala wa Israel katika Ukingo wa Magharibi?
Feb 16, 2026 00:05China sambamba na kuashiria kuidhinishwa kanuni mpya na baraza la mawaziri la usalama la Israel ili kuimarisha udhibiti wa Ukingo wa Magharibi, imeonya kuhusu matokeo mabaya ya hatua hiyo.
-
Israel yakasirishwa na kauli ya kumdhalilisha rais wake iliyotolewa na Trump
Feb 14, 2026 23:56Duru zilizo karibu na rais wa utawala wa kizayuni wa Israel zimeyaelezea matamshi ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kumtusi na kumdhalilisha rais wa utawala huo Isaac Herzog kuwa ni uvukaji mistari myekundu.
-
Umoja wa Afrika: Mateso dhidi ya Wapalestina lazima yakomeshwe
Feb 14, 2026 23:20Mahmoud Ali Youssouf Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) amesema kuwa, mauaji dhidi ya wananchi wa Palestina ni lazima yakomeshwe. Mahmoud Ali Youssouf alisema hayo jana (Jumamosi) wakati akiufungua mkutano wa kilele wa 39 wa umoja huo.
-
Zaidi ya raia 2,000 wa UK wamepigana kwa niaba ya Israel katika mauaji ya halaiki Gaza
Feb 12, 2026 22:32Maelfu ya raia wa Uingereza wamehudumu katika jeshi la Israel wakati wa vita vya mauaji ya halaiki vya utawala huo wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Katika upeo wa unyama, Israel imetumia silaha 'zilizoyeyusha' maelfu ya Wapalestina Ghaza
Feb 11, 2026 23:02Uchunguzi uliofanywa na televisheni ya Al Jazeera ya Qatar umefichua kuwa, utawala wa kizayuni wa Israel umetumia silaha zilizopigwa marufuku kimataifa zenye joto kupindukia katika vita vya mauaji ya kimbari huko Ghaza, na kupelekea "kuyeyuka" maelfu ya miili ya Wapalestina.
-
Kusimama kidete Somalia dhidi ya mpango hatari wa Wazayuni huko Somaliland
Feb 10, 2026 09:25Somalia imeuonya utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu kuwahamisha kwa lazima wa Wapalestina na kuwapeleka Somaliland ambalo limejitangazia uhuru.
-
Israel yaendelea kumwaga damu za Wapalestina, yaua 20 Gaza
Feb 04, 2026 06:53Mashambulizi mapya ya kinyama ya utawala wa Kizayuni wa Israel yamewaua shahidi watu wasiopungua 20, wakiwemo watoto wadogo katika Ukanda wa Gaza.
-
ANC yamkosoa Mfalme wa Afrika Kusini kwa kuwaalika maafisa wa Israel
Feb 04, 2026 06:53Chama tawala cha African National Congress (ANC) kimemkosoa vikali Mfalme wa Afrika Kusini, Buyelekhaya Dalindyebo kufuatia uamuzi wake tata wa kuwaalika maafisa kutoka Ubalozi wa Israel kutembelea hospitali za umma katika mkoa wa Eastern Cape. Dalindyebo ni mfalme wa watu wa AbaThembu, mojawapo ya jamii kubwa zaidi za kitamaduni za Afrika Kusini.