Pars Today
Mhariri wa gazeti moja nchini Misri ambaye pia ni mwandishi wa habari maarufu nchini humo, ameielezea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa nchi yenye nafasi chanya na yenye nguvu katika eneo la Mashariki ya Kati.
Katika siku za hivi karibuni walimwengu wameshuhudia mlolongo wa hujuma za kigaidi kuanzia Lebanon mpaka Iraq na kisha Syria, Bangladesh, baadhi ya maeneo ya Afrika na hata nchini Saudi Arabia.
Naibu Mkuu wa majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, haki za binadamu za Kimarekani zinatambulisha ujahili wa kisasa na ambao unachukiwa na fikra za waliowengi ulimwenguni.
Marasimu ya mwaka wa 27 wa kukumbuka kufariki dunia Imam Khomeini (MA) mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yalifanyika jana usiku katika nchi mbalimbali duniani.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Ismail Najar, amesema wafanyaziara milioni moja na laki saba na nusu wa ndani na kutoka nje ya nchi watashiriki kwenye Hauli ya Imam Khomeini (ra) itakayofanyika hapo kesho.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani matamshi ya kuivunjia heshima Iran yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, vitisho vya Marekani haviwezi kuifanya Iran isalimu amri mbele ya matakwa ya kutotosheka ya Washington
Rais Hassan Rouhani amesema utawala unaotokana na ridhaa ya wananchi ni moja ya fahari kubwa kwa Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kuimarishwa uhusiano kati ya Iran na India ni kwa maslahi ya usalama na ustawi wa kiuchumi wa eneo.
Luteni Kamanda wa Jeshi la Nchi Kavu la Iran amesema kuwa, jeshi hilo liko imara katika kuyalinda Mapinduzi ya Kiislamu na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.