-
Ombi la Guterres kwa nchi mbalimbali kufanya juhudi za pamoja ili kuyalinda mapatano ya JCPOA
Sep 17, 2020 04:20Baada ya Marekani kujitoa kwa upande mmoja katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA mwezi Mei mwaka 2018 hivi sasa nchi wanachama zilizosalia katika kundi la 4+1 zinasisitiza kuendelea kuwepo mapatano hayo kinyume na mtazamo wa Washington ambayo ilitaka kuchukuliwa hatua sawa na hiyo kutoka kwa wanachama wengine wa kundi la 5+1. Hvi sasa Marekani inafanya njama zake zote kujaribu kuyasambaratisha mapatano hayo ya JCPOA.
-
Iran: Makubaliano yoyote hayatodumu mpaka yatekeleze sawa haki na majukumu
Sep 16, 2020 21:52Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya haki za kimataifa amesema kuwa, makubaliano yoyote yale ya kimataifa hayawezi kudumu bila ya kuweko mlingano sawa katika utekelezaji wa haki na majukumu, na kwamba mapatano ya nyuklia ya JCPOA nayo hayawezi kutoka kwenye msingi huo.
-
Kukiri Biden kufeli siasa za Trump mbele ya Iran
Sep 15, 2020 02:51Huku wakati wa kufanyika uchaguzi wa Rais wa mwezi Novemba 2020 ukizidi kukabiria nchini Marekani, wagombea wawili wa uchaguzi huo, yaani rais wa hivi sasa Donald Trump na mpinzani wake Joe Biden wa chama cha Democrats kila mmoja amekuwa akitangaza misimamo yake kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo misimamo yao kuhusu Iran na mapatano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Sisitizo la Troika ya Ulaya la kutokuwa na itibari jaribio la Marekani la kutaka kurejesha vikwazo dhidi ya Iran
Sep 12, 2020 02:54Baada ya kugonga mwamba hatua za kila aina ilizojaribu kuchukua Marekani ili kurefusha vikwazo vya silaha dhidi ya Iran, Washington iliibua dai la kutaka kurejesha vikwazo vya kimataifa dhidi ya Tehran, ambavyo viliondolewa baada ya kufikiwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA;
-
Russia na China zapongeza kikao cha Kamisheni ya Pamoja ya JCPOA
Sep 02, 2020 03:31Russia na China zimepongeza mkutano wa Kamisheni ya Pamoja ya JCPOA uliofanyika jana Jumanne huko Vienna, mji mkuu wa Austria.
-
Araqchi: Wanachama wa JCPOA hawaitambui Marekani kama mshirika wao
Sep 01, 2020 23:01Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesema nchi zilizosalia katika makubaliano ya nyuklia ya Iran haziitambui Marekani kuwa mwanachama au mshirika wa mapatano hayo ya kimataifa.
-
Umbumbumbu wa Marekani katika masuala ya sheria, wameshindwa na sasa wanatoa vitisho
Aug 29, 2020 05:48Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amekosoa jitihada zinazofanywa na Marekani kwa ajili ya kurejesha vikwazo vya kimataifa dhidi ya Iran kuanzia tarehe 20 Oktoba mwaka huu wa 2020 na kusema: Viongozi wa serikali ya Marekani ni mbumbumbu katika masuala ya sheria na hawajui lolote kuhusiana na tendaji wa Umoja wa Mataifa.
-
Taarifa ya pamoja ya Tehran; nia njema ya Iran na matarajio ya Tehran kwa IAEA
Aug 27, 2020 05:12Baada ya mazungumzo ya kina ya siku mbili ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) mjini Tehran, Iran na wakala huo wamefikia makubaliano kuhusu namna ya kutatua masuala mbalimbali kwa nia njema.
-
Upinzani wa wanachama 13 wa Baraza la Usalama kwa ombi la Marekani la kuanzisha utaratibu wa "Snapback Mechanism"
Aug 22, 2020 05:57Kushindwa Marekani katika njama zake za kulazimisha kukubaliwa pendekezo la kuiongezea Iran muda wa vikwazo vya silaha katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kumeipelekea Washington kuchukua hatua ya kukurupuka ya kuwasilisha ombi la kuanzisha utaratibu wa kurejesha vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran papo kwa hapo yaani "Snapback Mechanism." Ombi hilo la Marekani hata hivyo nalo limepingwa vikali ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
JCPOA na utaratibu wa "Snapback Mechanism", Marekani katika mkwamo wa Baraza la Usalama
Aug 21, 2020 22:26Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amepinga hatua inayokiukaji sheria ya Marekani ya kutaka kutumia vibaya taratibu zilizowekwa kwenye makubaliano ya nyuklia ya JCPOA za kurejesha upya vikwazo vya silaha dhidi ya Iran.