Feb 17, 2020 13:01
Umoja wa Ulaya na Troika ya Ulaya inayojumuisha Ujerumani, Ufaransa, na Uingereza ni pande ambazo zimekuwa na nafasi muhimu katika kufikiwa mapatano ya nyuklia ya Iran yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA). Lakini baada ya Markenai kujiondoa katika mapatano hayo, pande hizo hazijachukua hatua za kivitendo kuyalinda na sasa hata maafisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Ulaya wamekiri kuhusu udhaifu huo.