-
Russia: Marekani itahatarisha usalama wa dunia ikijiondoa JCPOA
Oct 14, 2017 00:48Russia imeonya kuwa Marekani itahatarisha usalama wa dunia ikijiondoa katika mapatano ya nyuklia ya Iran yaliyotiwa saini mwaka 2015 baina ya Iran na madola sita makubwa duniani.
-
Larijani: Iran haitoinasa kwenye utando wa buibui wa Marekani
Oct 13, 2017 04:30Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema muamala wa wanasiasa wa Marekani ni wa kuvutia watu wa kawaida na wa mpito na akasisitiza kwa kusema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inafuatilia kwa makini mienendo na hatua zao zote na itachukua uamuzi kulingana na maslahi yake ya taifa.
-
John Kerry: Trump anasema uongo kuhusu makubaliano ya nyuklia ya JCPOA
Oct 13, 2017 04:05Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry ameukosoa vikali msimamo hasi ambao unatazamiwa kutangazwa na rais wa nchi hiyo Donald Trump kuhusiana na makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa kati ya Iran na nchi zinazounda kundi la 5+1.
-
Velayati: Kundi la 5+1 liilazimishe Marekani itekeleze majukumu yake kuhusu JCPOA
Oct 12, 2017 10:40Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Katika Masuala ya Kimataifa amesema kuwa Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) si makubaliano ya pande mbili ambayo Wamarekani wanaweza kuyafuta wao wenyewe.
-
Makubaliano ya nyuklia ya JCPOA; mtihani kwa Trump na itibari ya Marekani kimataifa
Oct 12, 2017 10:16Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA kwa kifupi, ni mtihani muhimu kwa serikali zilizoshiriki katika mazungumzo ya nyuklia na tawala nyingine duniani na kwamba, kutekeleza ahadi ni msingi wa dunia kuiamini serikali fulani.
-
EU: Marekani itajipotezea itibari kimataifa ikijiondoa katika mapatano ya nyuklia ya Iran
Oct 12, 2017 03:35Mkuu wa Sera za Kigeni katika Umoja wa Ulaya amesema iwapo Marekani itajiondoa katika mapatano ya nyuklia ya Iran yanayojulikana kama "Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji (JCPOA), jambo hilo litaipotezea Marekani itibari miongoni mwa nchi zingine duniani.
-
Rouhani: Iwapo Marekani itajitoa katika JCPOA madhara ya jambo hilo litaidhuru Marekani yenyewe
Oct 11, 2017 13:23Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, iwapo Marekani itajitoa katika makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kwa jina maarufu la JCPOA, madhara ya kujitoa huko yatawakumba Wamarekani wenyewe. Amesisitiza kuwa, Iran haitakwamishwa na jambo lolote katika kufikia malengo yake.
-
Uingereza yamtaka Trump aheshimu JCPOA
Oct 11, 2017 04:48Waziri Mkuu wa Uingereza amekariri kuwa London itaendelea kufungamana na kutekeleza makubaliano ya nyuklia ya Iran, huku akimtaka Rais Donald Trump wa Marekani kuheshimu mapatano hayo ya kimataifa.
-
Kuendelea upinzani sambamba na uamuzi tarajiwa wa Trump kuhusiana na makubaliano ya JCPOA
Oct 10, 2017 23:02Sambamba na kukaribia tarehe ya kutangazwa msimamo wa serikali ya Marekani kuhusiana na Iran na makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA), mazungumzo kwa ajili ya Washington kuheshimu makubaliano hayo ya nyuklia nayo yameshika kasi.
-
Zarif: Iran inataka suluhu, uthabiti na usalama katika eneo
Oct 10, 2017 13:20Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema, kwa muda sasa eneo la Mashariki ya Kati limekumbwa na machafuko na ukosefu wa uthabiti baada ya vikosi vya kijeshi vya kigeni kuanza kuingilia masuala ya eneo hili na amesisitiza kwamba Tehran inataka suluhu, uthabiti na amani vitawale katika mataifa yote ya eneo hili.