Velayati: Kundi la 5+1 liilazimishe Marekani itekeleze majukumu yake kuhusu JCPOA
(last modified Thu, 12 Oct 2017 14:10:21 GMT )
Oct 12, 2017 14:10 UTC
  • Velayati: Kundi la 5+1 liilazimishe Marekani itekeleze majukumu yake kuhusu JCPOA

Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Katika Masuala ya Kimataifa amesema kuwa Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) si makubaliano ya pande mbili ambayo Wamarekani wanaweza kuyafuta wao wenyewe.

Dakta Ali Akbar Velayati amesema kuwa hatua itakayochukuliwa na Rais Donald Trump wa Marekani kuhusiana na JCPOA haitabiriki na kwamba Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) umethibitisha mara nane kuwa Iran imeheshimu na kutekeleza majukumu yake kuhusu makubaliano hayo. Amesema hakuna mtu anayepasa kuwa marejeo kwamba Iran imeheshimu au imekiuka makubaliano hayo.  

Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Katika Masuala ya Kimataifa amesema kuwa, hakuna shaka kwamba viongozi wa Marekani wametekeleza kila hatua; na Iran pia itatoa jibu mkabala na hatua hizo za Marekani ili kulinda haki yake hiyo. 

Dakta Velayati amesisitiza kuwa makubaliano ya JCPOA yalipasishwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na hivi sasa makubaliano hayo yanatambuliwa kuwa ya kimataifa. Ameongeza kuwa, wanachama wengine wa kundi la 5+1 wanapasa kuilazimisha Marekani isikengeuke fremu iliyoainishwa na wakala wa IAEA na mazungumzo  ya JCPOA. 

Pande husika katika makubaliano ya kati ya Iran na kundi la 5+1 

Rais wa Marekani hadi kufikia mwishoni mwa wiki hii licha ya kutazamiwa kutangaza msimamo wake kuhusu makubaliano ya JCPOA sambamba na kutangaza stratejia ya nchi yake, anatarajiwa pia kuchukua hatua mpya dhidi ya Iran likiwemo Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah).

 

Tags