-
Alkhamisi, 24 Desemba, 2020
Dec 24, 2020 03:32Leo ni Alkhamisi tarehe 9 Mfunguo Nane Jamadil-Awwal 1442 Hijria ambayo inasadifiana na tarehe 24 Desemba 2020 Miladia.
-
Uingiliaji wa kigeni nchini Libya; chanzo cha kuvunjika mazungumzo ya amani
Dec 18, 2020 02:49Uingiliaji wa nchi za nje katika masuala ya ndani ya Libya unaendelea katika hali ambayo duru mpya ya mazungumzo ya amani ya nchi hiyo imevunjika kutokana na tofauti zilizoibuka kuhusu namna ya kuwachagua wanachama wa baraza la mawaziri.
-
Baraza la Usalama lataka mamluki wote waondoke nchini Libya
Dec 17, 2020 04:37Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa mwito wa kuondoka mara moja mamluki na wapiganaji wote wa nchi ajinabi nchini Libya.
-
Mazungumzo ya kisiasa ya Libya yakwama; pande hasimu zashindwa kuchagua serikali ya mpito
Dec 16, 2020 07:50Jitihada za timu ya wawakilishi wa amzungumzo ya kisiasa huko Libya zimeshindwa kuzaa matunda kwa mara nyingine tena baada ya kushindwa kuchagua serikali.
-
Waziri wa Ulinzi wa Libya: Hatua ya Ufaransa ya kumuunga mkono Khalifa Haftar ni aibu na fedheha
Dec 12, 2020 11:19Waziri wa Ulinzi wa Serikali ya Maafikiano ya Kitaifa ya Libya amesema kuwa, kitendo cha Ufaransa cha kumuunga mkono jenerali Khalifa Haftari kiongozi wa wanamgambo wanaojiita Jeshi la Taifa la Libya ni cha aibu na fedheha.
-
Hatua mpya ya utatuzi wa mgogoro wa Libya; maafikiano kuhusu namna ya kuwachagua viongozi wakuu wa serikali
Dec 09, 2020 12:54Awamu muhimu ya vita vya ndani vya Libya ilianza kwa shambulio la mwezi Aprili 2019 lililofanywa na kundi linalojiita Jeshi la Taifa la Libya (LNA) linaloongozwa na Khalifa Haftar ambalo shabaha yake ilikuwa ni kuudhibiti mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli na kuiangusha Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa (GNA); na wigo wa vita hivyo ukapanuka zaidi kwa uingiliaji wa pande za kigeni zinazounga mkono mirengo miwili hiyo.
-
Mjumbe wa UN: Libya ina "hali mbaya sana" kwa kuendelea kuwepo wapiganaji 20,000 wa kigeni
Dec 03, 2020 07:29Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya ametahadharisha kuwa, kuwepo wapiganaji na mamluki wasiopungua 20,000 wa kigeni nchini humo kunaifanya "hali iwe mbaya sana" huku silaha zikiendelea kumiminika pia katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini iliyoharibiwa vibaya na vita.
-
Walibya wakubaliana kuitisha kikao kingine; safari hii ndani ya Libya
Nov 26, 2020 11:00Wawakilishi wa makundi mbalimbali ya Libya wanaoshiriki katika kikao cha mjini Tangier, Morocco, wamekubaliana kuitisha kikao kingine katika mji wa Gadamis ndani ya Libya ili kujadiliana suala la kuunganisha mabunge ya nchi hiyo.
-
Wahajiri 74 wafariki dunia katika ajali mbaya ya baharini iliyotokea kwenye pwani ya Libya
Nov 13, 2020 08:05Shirika la Kimataifa la Uhajiri (IOM) limesema, wahajiri wasiopungua 74 wamefariki dunia baada ya chombo walichosafiria kuzama katika ajali mbaya iliyotokea kwenye pwani ya Khoms nchini Libya.
-
Mazungumzo ya Tunis na makubaliano ya kuitisha uchaguzi nchini Libya
Nov 13, 2020 01:34Mazungumzo baina ya pande mbalimbali za Libya yanaendelea Tunis, mji mkuu wa Tunisia kwa kusimamiwa na Umoja wa Mataifa. Lengo la mazungumzo hayo ni kuleta amani ya kudumu katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika. Taarifa za karibuni kabisa zinasema kuwa, washiriki wa mazungumzo hayo wamefikia makubaliano ya kuitisha uchaguzi nchini Libya katika kipindi kisichopindukia miezi 18 ijayo.