-
Baada ya kushindwa kutatua mgogoro wa Libya, Arab League yasema inasikitishwa na mapigano wakati huu wa kushughulikia corona
Apr 05, 2020 02:52Baada ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) kushindwa kutatua mgogoro wa Libya na kukomesha mapigano katika nchi hiyo ya Kiarabu ya kaskazini mwa Afrika, Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo ameishia kusema anasikitishwa na vita vinavyoendelea huko Libya badala ya kuelekezwa nguvu katika kupambana na ugonjwa wa COVID-19.
-
Uingiliaji wa moja kwa moja wa Uturuki katika masuala ya ndani ya Libya
Apr 03, 2020 10:50Licha ya matamshi ya hivi karibuni ya Rais Recep Tayyip Erdogan ya kutangaza kukomeshwa vita vyote vya nchi hiyo katika eneo hili na duniani kiujumla kutokana na wimbi la kuenea kirusi cha corona, lakini kuna taarifa mpya zinazosema kuwa jeshi la Uturuki linaingilia moja kwa moja masuala ya ndani ya Libya.
-
Kuanza operesheni ya "Dhoruba ya Amani" ya vikosi vya Serikali ya Maafikiano ya Kitaifa ya Libya dhidi ya wapiganaji wa Haftar
Mar 27, 2020 02:34Licha ya mgogoro wa virusi vya Corona na takwa la jamii ya kimataifa la kusimamishwa vita katika mataifa yenye mapigano na machafuko, lakini vikosi vya Serikali ya Maafikiano ya Kitaifa ya Libya vimeanzisha operesheni mpya iliyopewa jina la "Dhoruba ya Amani" dhidi ya wapiganaji wa kundi linalojiita Jeshi la Taifa la Libya (LNA) linaloongozwa na jenerali muasi Khalifa Haftar.
-
Vikosi vya GNA Libya vyaanzisha operesheni ya "Dhoruba ya Amani" dhidi ya wapiganaji wa Haftar
Mar 26, 2020 08:04Vikosi vya jeshi la Serikali ya Maafikiano ya Kitaifa ya Libya (GNA) vimetangaza kuwa vimeanzisha operesheni iliyopewa jina la "Dhoruba ya Amani" dhidi ya wapiganaji wa kundi linalojiita Jeshi la Taifa la Libya (LNA) linaloongozwa na Khalifa Haftar.
-
Kukaribisha Umoja wa Mataifa makubaliano ya usitishaji vita katika vita vya ndani nchini Libya
Mar 24, 2020 13:30Vita vya ndani nchini Livya viliibua wasiwasi mkubwa kufuatia mashambulio ya mara kwa mara ya Jeshi la Taifa la Libya linaloongozwa na jenerali Khalifa Haftar yaliyoanza Aprili mwaka jana kwa shabaha ya kuiangusha Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa.
-
Wapiganaji wa Haftar wapuuza mwito wa UN, waendelea kumwaga damu Libya
Mar 24, 2020 07:58Serikali ya Maafikiano ya Kitaifa ya Libya imetangaza habari ya kuuawa watu 6 katika mashambulizi ya roketi ya kundi la wanamgambo linalojiita jeshi la kitaifa la Libya linaloongozwa na Jenerali muasi Khalifa Haftar jana Jumatatu viungani mwa mjini mkuu Tripoli.
-
Tripoli yaitaka Khartoum kuwaondoa mamluki wa Kisudani nchini Libya
Mar 21, 2020 11:47Mjumbe katika Baraza la Utawala la Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa nchini Libya, Muhammad Ammari amesema Libya ingali inasubiri ufafanuzi wa Serikali ya Sudan kuhusu uwepo wa mamluki wa Kisudani katika safu za wapiganaji wa jenerali muasi, Khalifa Haftar wanaoendelea kuhujumu mji wa Tripoli.
-
UN yalaani mauaji ya wasichana na wanawake mjini Tripoli, Libya
Mar 20, 2020 12:06Umoja wa Mataifa umelaani shambulizi la mabomu katika mji mkuu wa Libya Tripoli, ambalo liliua na kujeruhi watoto wa kike na wanawake kadhaa.
-
Watoto 3 wauawa katika shambulizi la wapiganaji wa Haftar Libya
Mar 19, 2020 07:52Watoto watatu wa familia moja wameuawa baada ya kundi la wanamgambo kwa jina la jeshi la kitaifa la Libya linaloongozwa na Jenerali muasi Khalifa Haftar kulishambulia kwa mabomu eneo la Ain Zara, kusini mwa mji mkuu wa Libya, Tripoli.
-
Wahajiri 400 wakamatwa wakijaribu kwenda Ulaya na kurejeshwa Libya
Mar 16, 2020 02:33Shirika la Kimataifa la Wahajiri (IOM) limesema Gadi ya Pwani ya Libya imewakamata wahajiri 400 wakiwa safarini kuelekea Ulaya na kuwarejesha katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli.