-
Mashtaka rasmi ya Russia kwa Umoja wa Mataifa kuhusu maabara za silaha za kibiolojia za Marekani nchini Ukraine
Oct 28, 2022 22:54Russia imepeleka malalamiko yake rasmi kwa Umoja wa Mataifa kuhusu kuwepo kwa maabara za silaha za kibiolojia za Marekani nchini Ukraine. Vasily Nebenzia, mwakilishi wa kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa, amethibitisha kwamba nchi yake imekusanya ushahidi wa kutosha kuhusu uwepo wa maabara ya silaha hizo za kibiolojia za Marekani huko Ukraine.
-
Russia: Kuwepo kikosi cha jeshi la Marekani nchini Romania ni tishio kubwa
Oct 27, 2022 09:48Ikulu ya Rais wa Russia, Kremlin, imetangaza kuwa kupelekwa kwa wanajeshi wa Marekani nchini Romania, karibu na mpaka wa Ukraine, ni tishio kwa Russia. Hatua hiyo imechukuliwa na Marekani zaidi ya miezi minane baada ya Moscow kuanza mashambulizi ya kijeshi nchini Ukraine.
-
Iran: Uungaji mkono wa Magharibi kwa Israel ni mfano mkubwa zaidi wa ukiukaji wa haki za binadamu
Oct 26, 2022 03:41Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amelaani shambulio la utawala ghasibu wa Israel katika mji wa Nablus katika Ukingo wa Magharibi huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu, na kuutaja uungaji mkono usio na kikomo wa Marekani na nchi nyingine za Magharibi kwa utawala dhalimu wa Israel kuwa ni kielelezo kikubwa zaidi cha ukiukwaji wa haki za binadamu.
-
Iran: Vikwazo kwa wazalishaji gesi kuwa na matokeo hasi
Oct 25, 2022 23:02Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametahadharisha kuwa, hatua ya Wamagharibi ya kuziwekea vikwazo nchi zinazozalisha na kuuza nje ya nchi gesi itakuwa na matokeo hasi yasiyoweza kurekebishika.
-
Hizbullah: Saudia na Marekani zinakwamisha uchaguzi wa Rais wa Lebanon
Oct 25, 2022 07:29Afisa mwandamizi wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema balozi za Saudi Arabia na Marekani jijini Beirut zimekula njama na kuweka vizingiti vya kila aina ili kukwamisha uchaguzi wa rais, huku ikiwa imesalia wiki moja tu kabla ya kumalizika muhula wa Rais Michel Aoun wa nchi hiyo.
-
Maandamano ya kupinga siasa za Marekani nchini Ethiopia
Oct 25, 2022 06:27Sambamba na kushtadi mapigano nchini Ethiopia na kuvunjwa makubalianao ya usitishaji vita ya miezi mitano na kuwaka tena moto wa vita katika nchi hiyo, maelfu ya Waethiopia walifanya maandamano ya nchi nzima siku ya Jumamosi kulaani uingiliaji wa madola ya kigeni, hasa Marekani, katika masuala ya ndani ya nchi yao.
-
Hujuma za magaidi zaongezeka kwa 300% Afrika licha ya operesheni za US
Oct 24, 2022 00:32Ripoti mpya ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) inaonesha kuwa, mashambulizi ya magenge ya wanamgambo yameongezeka kwa asilimia 300 katika nchi za Afrika katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.
-
Uchunguzi wa maoni: Mfumuko wa bei na uhalifu ndio maswala makuu yanayowashughulisha zaidi Wamarekani
Oct 23, 2022 01:06Matokeo ya uchunguzi mpya wa maoni yanaonyesha kwamba mfumuko wa bei na takwimu za juu za uhalifu nchini Marekani ndizo mambo yanayowatia wasiwasi mkubwa zaidi Wamarekani.
-
Iran: Hatutaipatia Marekani fursa yoyote ya ziada katika mazungumzo ya uondoaji vikwazo
Oct 22, 2022 09:05Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema, Iran inachukua hatua kwa kutumia mantiki na kuchunga mistari myekundu ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na haitapatia Marekani fursa yoyote ya ziada katika mazungumzo ya uondoaji vikwazo.
-
Kukiri Borrell juu ya mwisho wa udhibiti wa Marekani na nafasi isiyokuwa athirifu ya Ulaya duniani
Oct 22, 2022 07:41Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell amekiri katika mahojiano yake siku ya Alhamisi iliyopita kwamba tunaishi katika ulimwengu wa kambi kadhaa na kwamba kipindi cha udhibiti wa upande mmoja wa Marekani kimefikia tamati.