-
Marekani yakiri kuhusu nguvu ya Iran ya ndege zake zisizo na rubani (droni)
Apr 21, 2021 22:22Jenerali Kenneth McKenzie, Kamanda wa Kamandi Kuu ya askari wa kigaidi wa Marekani CENTCOM, amekiri kwamba nguvu ya droni za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepunguza na kudhoofisha pakubwa uwezo wa anga wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati).
-
Sanders ataka kubanwa misaada ya Marekani kwa utawala wa Kizayuni wa Israel
Apr 21, 2021 05:07Seneta wa kujitegemea wa Marekani, Bernie Sanders ameitaka serikali ya nchi hiyo kubana misaada yake kwa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa shabaha ya kuushinikiza ukomeshe kukalia kwa mabavu ardhi ya Palestina.
-
Askari polisi aliyemuua Mmarekani mweusi, George Floyd apatikana na hatia
Apr 21, 2021 01:29Derek Chauvin, afisa mzungu wa polisi wa Marekani ambaye alimuua kikatili Mmarekani mwenye asili ya Afrika, George Floyd na kuzusha maandamano makubwa ya kupinga ubaguzi wa rangi dunia nzima hatimaye amepatikana na hatia katika mashitaka yote ya mauaji yaliyokuwa yakimuandama.
-
Balozi wa Marekani nchini Russia aitwa kurejea nyumbani
Apr 20, 2021 03:50Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imetangaza kwamba imemtaka balozi wake aliyeko mjini Moscow Russia arejee nyumbani kwa mashauriano zaidi na viongozi wa Washington.
-
Rais wa Afghanistan: Taifa letu halitaporomoka kwa kuondoka askari wa Marekani
Apr 19, 2021 03:14Rais Ashraf Ghani wa Afghanistan ameashiria uamuzi uliotangazwa hivi karibuni na Rais wa Marekani Joe Biden wa kuwaondoa askari wa jeshi la nchi hiyo walioko nchini Afghanistan na kusisitiza kuwa, taifa hilo kamwe halitaporomoko kwa kuondoka wanajeshi hao vamizi wa US.
-
Janga la ukatili wa utumiaji silaha nchini Marekani na indhari mpya ya Biden
Apr 18, 2021 21:56Rais Joe Biden wa Marekani Ijumaa usiku alitoa taarifa na kulaani ufyatulianaji risasi ulioandamana na mauaji katika mji wa Indianapolis na kusema: "Kila siku idadi kubwa ya watu wanapoteza maisha kutokana na ukatili wa utumiaji silaha. Sisi tunapaswa kuchukua hatua za kuokoa maisha." Biden alikiri kuwa, ukatili wa utumiaji silaha sasa ni janga nchini Marekani.
-
Hatua mpya za serikali ya Biden dhidi ya Russia; vikwazo vipya na kufukuzwa wanadiplomasia
Apr 17, 2021 07:40Serikali ya Marekani juzi Alhamisi iliwawekea vikwazo Shakhsia 12 wa serikali ya Russia wakiwemo viongozi kadhaa wa serikali, wa masuala ya intelijensia wa nchi hiyo pamoja na taasisi 20 za Russia.
-
Russia yawafukuza wanadiplomasia 10 wa Marekani kujibu vikwazo vya Washington
Apr 16, 2021 22:59Katika kujibu mapigo kwa hatua ya uhasama na vikwazo vipya vya Washington vilivyotangazwa hivi karibuni na Rais Joe Biden dhidi ya Russia, serikali Moscow imewatimua nchini humo wanadiplomasia kumi wa Marekani.
-
Russia yaahidi kujibu mapigo baada ya kuwekewa vikwazo vipya vya Marekani
Apr 16, 2021 07:35Russia imeikosoa vikali serikali ya Marekani ikisema kuwa itajibu mapigo kwa vikwazo vipya vya nchi hiyo vilivyotangazwa na Rais Joe Biden dhidi ya Moscow.
-
Mtazamo wa Kiongozi Muadhamu kuhusu mazungumzo ya nyuklia; sharti la Iran, msingi wa kuhuishwa JCPOA
Apr 15, 2021 23:05Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, siasa za Iran kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ziko wazi, na maafisa wanaoshiriki kwenye mazungumzo ya kuhuishwa makubaliano hayo wanapaswa kuwa macho ili yasirefushwe kupita kiasi, suala ambalo lina madhara kwa taifa.