-
Israel yatishia kuishambulia Iran iwapo Biden atairejesha US katika JCPOA
Jan 15, 2021 10:34Mpambe wa karibu wa Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni ametishia kuwa huenda Israel ikaishambulia kijeshi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iwapo serikali ijayo ya Marekani itarejea katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Marekani yakataa ombi la Umoja wa Mataifa la kuitaka ifutilie mbali vikwazo dhidi ya Ansarullah
Jan 15, 2021 09:22Ikiwa ni katika juhudi zake za kuunga mkono muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya Yemen, Marekani imechukua hatua ya kuiwekea vikwazo harakati ya Ansarullah. Hatua hiyo ambayo imechukuliwa katika siku za mwisho za utawala wa Rais Trump huko White House imekabiliwa na radiamali kali ya Umoja wa Mataifa.
-
Ukwamishaji mpya wa Marekani dhidi ya juhudi za Iran za kupambana na virusi vya corona
Jan 14, 2021 23:05Baada ya kujitoa katika mapatano ya kimataifa ya nyuklia mashuhuri kama JCPOA hapo mnamo Mei 2018, na katika fremu ya kile kinachotajwa kuwa 'mashinikizo ya juu kabisa', Marekani imekuwa ikitekeleza vikwazo vikali zaidi katika historia yake dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wala haijawahi kulegeza vikwazo hivyo vya kinyama hata katika kipindi hiki kigumu cha kuenea duniani virusi hatari vya corona.
-
Aswarullah: Muungano vamizi wa Yemen upate funzo kutokana na hali iliyomkumba Trump
Jan 14, 2021 04:28Msemaji wa harakati ya wananchi ya Answarullah ya nchini Yemen amesema kuwa, muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia unapaswa ujifunze kutokana na hali iliyo nayo hivi sasa serikali ya Donald Trump huko Marekani hasa kwa vile wavamizi hao wa Yemen waliitumainia sana serikali hiyo.
-
Mshauri wa Kiongozi Muadhamu: Marekani haiwezi kuihadaa Iran kwa pipi
Jan 13, 2021 23:38Mshauri wa ngazi ya juu wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Marekani sharti iiondolee Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vikwazo vyote na kwamba Tehran haitakubali kitu kingine ghairi ya hicho.
-
Russia yapuuzilia mbali bwabwaja mpya za Marekani dhidi ya Iran
Jan 13, 2021 23:09Russia imekosoa vikali madai ya kipropaganda ya Marekani ya kujaribu kulifungamanisha kundi la kigaidi la al-Qaeda na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pasi na kutoa ushahidi wowote.
-
Hillary Clinton akiri kuwa utawala wa Saudia ndio uliomuua Jamal Khashoggi
Jan 13, 2021 08:41Mgombea urais aliyeshindwa katika uchaguzi wa mwaka 2016 nchini Marekani amekiri kuwa utawala wa Saudi Arabia ndio uliomuua mwandishi wa habari Jamal Khashoggi aliyekuwa mkosoaji mkubwa wa utawala huo.
-
Iran yailaani Marekani kwa kuiweka Cuba katika orodha ya 'waungaji mkono ugaidi'
Jan 13, 2021 04:42Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali hatua ya Marekani kuiweka Cuba katika orodha ya nchi ambazo eti zinaunga mkono ugaidi. Iran aidha imesema inafungamana na Cuba katika mapamano yake dhidi ya madola ya kibeberu duniani.
-
Waziri wa Ulinzi: Maadui wameshindwa kupigisha magoti Iran
Jan 13, 2021 01:12Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Brigedia Jenerali Amiri Hatami amesisitiza kuwa, maadui walidhani wangeipigisha magoti Iran lakini wameshindwa kabisa kutokana na Wairani kusimama kidete dhidi yao na sasa ni Rais Trump wa Markeani na waitifaki wake ndio wanaochukiwa zaidi na watu duniani na watatupwa katika dampo la taka za historia.
-
Sana'a: Marekani ni kinara wa ugaidi wa kimataifa
Jan 12, 2021 09:43Msemaji wa Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen amesema kuwa Marekani imetumia njia zote kwa ajili ya kuliangamiza taifa la Yemen na nchi hiyo ndio kinara wa ugaidi duniani.