Wananchi Marekani hawaridhishwi serikali yao kupuuza suala la umaskini
https://parstoday.ir/sw/news/world-i67230-wananchi_marekani_hawaridhishwi_serikali_yao_kupuuza_suala_la_umaskini
Utafiti mpya wa maoni nchini Marekani unaonyesha kuwa, akthari ya wananchi hawaridhishwi na hatua ya serikali ya nchi hiyo ya kupuuza vita dhidi ya umaskini, kuboresha huduma za afya na elimu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 25, 2021 00:20 UTC
  • Wananchi Marekani hawaridhishwi serikali yao kupuuza suala la umaskini

Utafiti mpya wa maoni nchini Marekani unaonyesha kuwa, akthari ya wananchi hawaridhishwi na hatua ya serikali ya nchi hiyo ya kupuuza vita dhidi ya umaskini, kuboresha huduma za afya na elimu.

Utafiti huo mpya wa maoni uliofanywa na Hill-Harris X unaonyesha kuwa, akthari ya watu walioshiriki katika utafiti huo wa maoni wanaamini kuwa serikali ya Marekani imetumia pesa kidogo katika mapambano dhidi ya umaskini na katika kuboresha huduma za afya na elimu nchini humo. 

Matokeo ya utafiti huo wa maoni yanaonyesha kuwa, asilimia 58 ya Wademocrat, nusu ya wapiga kura na asilimia 38 ya Warepublican wanaojitegema wameeleza kuwa, serikali imetumia fedha kidogo sana kupunguza tathira za maambukizi ya kirusi cha corona.  

Wananchi wa Marekani wakiandamana kulalamikia usimamizi mbovu wa janga la corona 

Marekani ni kati ya nchi zilizo na idadi kubwa ya maambukizi ya corona na vifo vya ugonjwa huo duniani. Vilevile kushindwa serikali ya Marekani kusimamia vyema janga la corona pia kumeathiri pakubwa uchumi wa nchi hiyo.  

Wakati huo huo maelfu ya wakazi wa mji wa Houston katika jimbo la Texas nchini Marekani wameonekana wakiwa katika safu ndefu kwa masaa kadhaa wakisubiri kupewa misaada ya chakula kufuatia kukatika umeme na maji jimboni humo.