-
"Trump! Funga domo lako! Acha kuchochea moto wa ubaguzi! Acha kiu yako ya kumwaga damu"
May 31, 2020 03:42Mkuu wa Kamati ya Habari ya Baraza la Wawakilishi la Marekani ametoa onyo kali kwa rais wa nchi hiyo Donald Trump akimtaka afumbe domo lake, aache kuchochea moto wa ubaguzi wa rangi na kumwaga damu za watu wasio na hatia.
-
Zarif: Umefika wakati wa dunia kuungana katika kukabiliana na ubaguzi wa rangi
May 31, 2020 00:19Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma ujumbe katika mtandao wa Twitter akiashiria mauaji ya kusikitisha yaliyofanywa na polisi ya Marekani dhidi ya Mmarekani mweusi ambaye hakuwa na silaha ya aina yoyote katika mji wa Minneapolis na kusema: Umewadia wakati wa dunia kuungana kwa ajili ya kukabiliana na ubaguzi wa rangi.
-
India: Madai ya kufanyika mazungumzo ya simu kati ya Narendra Modi na Trump hayana msingi
May 31, 2020 00:11Serikali ya India imeyataja kuwa ya uongo madai ya Rais Donld Trump wa Marekani kwamba amefanya mazungumzo ya simu na Narendra Modi, Waziri Mkuu wa nchi hiyo kuhusiana na masuala ya mzozo wa mpaka kati yake na China.
-
China yalaani kitendo cha Marekani kukataa kutoa vibali vya kuingia nchi hiyo wanafunzi wa China
May 30, 2020 23:59Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amelaani kitendo cha Marekani kukataa kutoa vibali vya kuingia wanafunzi wa China katika nchi hiyo.
-
Cuba na Venezuala zalaani ukatili wa polisi wa Marekani dhidi ya watu weusi
May 30, 2020 23:52Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Cuba na Venezula wamelaani vikali ukatili wa polisi wa Marekani dhidi ya Wamarekani weusi pamoja na ujumbe wa kuchochea utumiaji mabavu alioutoa Rais Donald Trump.
-
Maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini Marekani, sababu na hatari zake
May 30, 2020 21:54Marekani imetumbukia tena katika machafuko makubwa kutokana na malalamiko ya wananchi wanaopinga mauaji yaliyofanywa na polisi wa nchi hiyo dhidi ya raia mweusi.
-
Hata serikali ya Canada nayo yasikitishwa na ukandamizaji wa polisi nchini Marekani
May 30, 2020 07:48Waziri Mkuu wa Canada amesema kuwa, nchi yake inafuatilia kwa sura ya kuemewa na woga maandamano na machafuko pamoja na ubaguzi wa rangi na ukandamizaji mkubwa unaofanywa na polisi wa Marekani.
-
Trump awatisha waandamanaji wanaolalamikia ukatili Polisi Marekani dhidi ya Wamarekani Weusi
May 30, 2020 03:44Ukatili usio na kikomo wa Jeshi la Polisi nchini Marekani dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika au Wamarekani weusi ambao unafanyika katika fremu ya sera jumla za ubaguzi wa rangi dhidi ya kaumu hiyo umeibua malalamiko makubwa katika siku za hivi karibuni nchini humo. Malalamiko hayo yameibuka baada ya Mmarekani mweusi kuuawa kinyama siku chache zilizopita mikononi mwa afisa wa polisi mzungu.
-
AU yalaani ukatili wa polisi ya Marekani dhidi ya raia weusi
May 30, 2020 03:44Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika amelaani vikali mauaji ya raia mweusi nchini Marekani katika jimbo la Minnesota, licha ya kuwa hakuwa na silaha yoyote.
-
EU, China zaikosoa US kwa kuondoa misamaha ya vikwazo vya nyuklia dhidi ya Iran
May 30, 2020 03:41Umoja wa Ulaya na China zimekosoa vikali hatua ya Marekani ya kufuta misamaha ya vikwazo inayohusiana na makubaliano ya kimataifa ya nyuklia ya Iran ya JCPOA.