-
EU yapinga njama za Trump dhidi ya Wapalestina
Feb 05, 2020 01:16Umoja wa Ulaya umepinga mpango uliopendekezwa na Rais Donald Trump wa Marekani ambao unakandamiza haki za taifa la Palestina uliopewa jina la "Muamala wa Karne" ukisisitiza kuwa, mpango huo unakanyaga sheria za kimataifa.
-
Mbunge wa Marekani akiri kuwa serikali ya Washington imetenda kosa kuwadadisi raia wa Iran
Feb 04, 2020 10:18Mbunge wa chama cha Democrat katika bunge la wawakilishi amekiri kwamba serikali ya nchi hiyo imefanya kosa katika kuwakamata na kuwadadisi raia wa Iran katika mipaka ya Marekani.
-
Pakistan: Matumaini ya Trump kuwa mpatanishi katika mgogoro wa Kashmir, ni ujinga mkubwa
Feb 03, 2020 12:24Seneta wa ngazi ya juu nchini Pakistan sambamba na kubainisha kwamba Marekani kamwe haijawahi kuwatakia jambo la kheri Waislamu, amesema kuwa Trump hataki hata kidogo kutatuliwa matatizo ya Waislamu wa Kashmir.
-
Arab League yapinga "Muamala wa Karne", yatoa onyo kali kwa Israel
Feb 02, 2020 07:28Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) wamepinga mpango eti wa amani uliopendekelezwa na Marekani kwa ajili ya mgogoro wa Wapalestina na utawala wa kizayuni wa Israel maarufu kwa jina la "Muamala wa Karne".
-
Mamia waandamana Tel Aviv na London kupinga 'Muamala wa Karne'
Feb 02, 2020 03:51Mamia ya watu wamefanya maandamano katika barabara za mji mkuu wa utawala haramu wa Israel, Tel Aviv kulaani "Muamala wa Karne" uliozinduliwa hivi karibuni na Rais Donald Trump wa Marekani, anayedai kuwa mapendekezo yaliyomo kwenye mpango huo ghalati yataleta suluhu ya amani ya mgogoro baina ya Israel na Palestina.
-
Baraza la Mamufti wa Russia: Nchi za Kiislamu ziungane kupambana na "Muamala wa Karne"
Feb 01, 2020 23:11Mkurugenzi wa Baraza la Mamufti wa Russia ambacho ndicho chombo kikubwa zaidi ya Kiislamu nchini humo amesema kuwa, kuna wajibu wa nchi zote za Kiislamu kuungana na kuwa kitu kimoja ili kupambana na mpango wa Kimarekani-Kizayuni wa "Muamala wa Karne."
-
IRGC: 'Majeraha ya Ubongo' ni njia ya kuficha idadi ya askari wa Marekani waliouawa katika hujuma ya makombora ya Iran
Feb 01, 2020 10:08Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema madai ya Marekani kuhusu idadi kubwa ya wanajeshi wake waliopata 'majeraha ya ubongo' kufuatia makombora ya Iran ya ulipizaji kisasi yaliyolenga kituo cha kijeshi cha Ain al Assad nchini Iraq ni njia ya kuficha idadi ya wanajeshi waliouawa katika oparesheni hiyo.
-
Kuvuka sekta ya nyuklia ya Iran vikwazo haramu na vya kidhalimu vya Marekani
Jan 31, 2020 21:46Wizara ya Fedha ya Marekani imeendeleza sera zake za ukiukaji sheria, zilizofeli na kugonga mwamba kwa kumwekea vikwazo Ali Akbar Salehi, Makamu wa Rais na Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI).
-
Waziri wa Trump afurahia virusi vya Corona, asema vitainua uchumi wa Marekani
Jan 31, 2020 21:45Waziri wa Biashara nchini Marekani Wilbur Ross amesema kwamba mripuko mbaya wa virusi vya Corona nchini China unaweza kuinua uchumi wa Marekani.
-
Wagombea wa urais Marekani wakosoa 'mpango wa amani' wa Trump
Jan 30, 2020 23:11Wagombea wa chama cha Democrat kwenye uchaguzi wa rais wa mwaka huu 2020 nchini Marekani wamekosoa vikali kile kinachotajwa kuwa mpango wa amani uliozinduliwa hivi karibuni na Rais Donald Trump wakisisitiza kuwa, pendekezo hilo lililopewa jina la wa 'Muamala wa Karne' halitakuwa na matokeo mengine ghairi ya kushadidisha mgogoro baina Palestina na Israel.