Arab League yapinga "Muamala wa Karne", yatoa onyo kali kwa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i58899-arab_league_yapinga_muamala_wa_karne_yatoa_onyo_kali_kwa_israel
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) wamepinga mpango eti wa amani uliopendekelezwa na Marekani kwa ajili ya mgogoro wa Wapalestina na utawala wa kizayuni wa Israel maarufu kwa jina la "Muamala wa Karne".
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 02, 2020 07:28 UTC
  • Arab League yapinga

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) wamepinga mpango eti wa amani uliopendekelezwa na Marekani kwa ajili ya mgogoro wa Wapalestina na utawala wa kizayuni wa Israel maarufu kwa jina la "Muamala wa Karne".

Taarifa ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Kiarabu baada ya mkutano wao mjini Cairo imetolewa muda mfupi baada ya Rais Mahmoud Abbas wa Palestina kukata uhusiano wote na utawala haramu wa Israel na serikali ya Marekani ukiwe uhusiano wa masuala ya usalama.

Taarifa ya Arab League imesema: 'Uamuzi wa kukataa na kupinga mpango wa Muamala wa Karne umepasishwa kwa sauti moja na mawaziri wote wa mambo ya nje wa nchi za Kiarabu kwa sababu mpango huo haukidhi hata matakwa ya chini kabisa ya taifa la Palestina na unapinga maazimio na sheria za kimataifa.'

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Kiarabu pia wameitahadharisha Israel isitekeleze vipengee vya mpango huo wa Donald Trump na kukiuka sheria za kimataifa na wameitaka jamii ya kimataifa ikabiliane na hatua yoyote ile ya kutekelezwa mpango huo.

Waingereza wakipinga Muamala wa Karne

Vilevile wametangaza uungaji mkono wao kamili kwa mapambano ya taifa la Palestina na viongozi wake.

Jumanne iliyopita Rais Donald Trump wa Marekani, akiwa pamoja na Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel, Benjamin Netanyahu katika ikulu ya White House, alizindua mpango wa kibaguzi uliopewa jina la "Muamala wa Karne" akidai kuwa ni fursa ya kutatua mgogoro wa Wapalestina na Israel.

Mpango huo wa kihaini unaokidhi matakwa ya utawala haramu wa Israel na kufuta haki za wananchi madhulumu wa Palestina, umeandaliwa na serikali ya Marekani kwa ushirikiano na maafikiano na baadhi ya nchi za Kiarabu ikiwemo Saudi Arabia, Bahrain na Imarati.