-
Waziri Mkuu wa Sudan aelekea Washington katika juhudi za kupigania nchi yake iondolewe vikwazo
Dec 01, 2019 23:07Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok ameelekea mjini Washington katika juhudi za kupigania nchi yake iondolewe vikwazo ilivyowekewa na Marekani na kuondolewa jina la nchi hiyo kwenye orodha ya wafadhili na waungaji mkono wa ugaidi.
-
Larijani: Watawala wa Marekani lazima wasitishe sera ya mashinikizo ya juu zaidi dhidi ya Iran
Dec 01, 2019 09:15Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, 'Bunge la Iran' amesema sera ya Marekani ya mashinikizo ya juu zaidi dhidi ya Iran ni ghalati na ni lazima watawala wa Marekani wasitishe sera hiyo.
-
Mwanachama wa Republican nchini Marekani ataka Ilhan Omar anyongwe
Dec 01, 2019 04:10Shirika la mtandao wa kijamii wa Twitter limelazimika kufuta akaunti za mgombea wa ubunge wa chama tawala cha Republican nchini Marekani, Danielle Stella kwa kuandika maneno ya kichochezi na kibaguzi dhidi ya Ilhan Omar, mbunge Muislamu katika Kongresi ya Marekani.
-
Wasiwasi unaoongezeka wa Wahafidhina kuhusu uingiliaji wa Donald Trump katika siasa za ndani za Uingereza
Dec 01, 2019 03:10Uingiliaji unaoongezeka kila siku wa Rais Donald Trump wa Marekani katika masuala ya ndani ya Uingereza hususan kwa kuzingatia kukaribia kufanyika uchaguzi wa kabla ya wakati wa Bunge la Uingereza siyo tu kwamba, umekabiliwa na ukosoaji wa chama cha upinzani cha Leba, bali filihali chama tawala cha Kihafidhina (Conservative) nacho kimeonyesha wasiwasi kilionao kuhusiana na suala hilo.
-
Trump, changamoto kubwa zaidi kwa Umoja wa Ulaya
Nov 30, 2019 01:01Tokea aingie madarakani mwezi Januari 2017, Rais Donald Trump wa Marekani amekuwa akitekeleza siasa za upande mmoja na kuiondoa nchi hiyo katika mitakaba muhimu ya kimataifa, kinyume kabisa na matarajio na mitazamo ya Umoja wa Ulaya na hivyo kupanua pengo la tofauti kati ya pande hizo mbili za Bahari ya Atlantiki.
-
Trump akutana na Rais Ashraf Ghani wa Afghanistan
Nov 29, 2019 07:44Katika safari yake ya ghafla nchini Afghanistan, Rais Donald Trump wa Marekani amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Ashraf Ghani wa nchi hiyo.
-
Macron: Siombi samahani, nakariri tena kwamba NATO imekufa ubongo
Nov 29, 2019 04:38Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amesema kuwa kauli yake kwamba Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) limepatwa na kifo cha ubongo ilipiga kengele ya hatari kwa nchi wanachama na kwamba hataomba radhi kwa kutoa matamshi hayo.
-
Kamanda wa zamani wa kikosi cha wanamaji wa Marekani akosoa vikali sera za Trump
Nov 28, 2019 23:05Kamanda wa jeshi la wanamaji katika Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) aliyepigwa kalamu nyekundu hivi karibuni, ameelezea uingiliaji wa Rais Donald Trump wa nchi hiyo katika hukumu za vyombo vya mahkama ya kijeshi kupitia jumbe zake za mtandao wa kijamii wa Twitter na kusema kuwa, hatua hiyo haijawahi kushuhudiwa huko nyuma.
-
China: Siasa za Marekani katika uga wa kibiashara zinabainisha malengo yake ya kishetani
Nov 28, 2019 23:02Serikali ya China imesisitiza kwamba hatua mbovu za baadhi ya viongozi wa Marekani kuihusu Beijing, zinabainisha malengo yao ya kishetani.
-
Trump alishauriana na Michel Temer kuivamia kijeshi Venezuela
Nov 28, 2019 06:55Rais wa zamani wa Brazil, Michel Temer, amesema kuwa, Rais wa Marekani alimuuliza kuhusu namna ya kuishambulia Venezuela.