-
Jihadul Islami: US na Isreal zinafuatilia malengo sawa Gaza
Mar 16, 2024 03:50Afisa wa ngazi ya juu wa Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina amesema pamoja na unafiki na hadaa za Marekani, lakini dola hilo la kiistikbari linafuatilia malengo yanayoshabihiana na ya Israel katika Ukanda wa Gaza.
-
Jaribio la Marekani eti la kusimamisha vita huko Gaza, mbinu ya kugeuza maoni ya umma
Mar 15, 2024 12:55Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amezungumzia matukio ya hivi karibuni katika eneo la Asia Magharibi hususan Ukanda wa Gaza na kueleza kuwa hakuna anayeamini madai ya Washington ya kujaribu kusimamisha vita vya Gaza.
-
Kurefushwa hali ya hatari kitaifa; muendelezo wa mtazamo wa uadui wa Marekani dhidi ya Iran
Mar 14, 2024 23:17Siku ya Jumanne, Rais Joe Biden wa Marekani alirefusha kwa mwaka mwingine mmoja, muda wa hali ya hatari ya kitaifa kuhusu Iran. Tangu 1995, marais wote wa Marekani wamekuwa wakirefusha kila mwaka hali hiyo iliyoanza kutekelezwa kupitia Agizo la Utendaji nambari 12957 dhidi ya Iran.
-
Wajumbe wa Baraza la Seneti wamtaka Biden aache kuipatia Israel msaada wa silaha
Mar 13, 2024 07:16Wajumbe wa Baraza la Seneti la Marekani wamemuandikia barua Rias wa nchi hiyo Joe Biden wakimtaka aache kuipatia silaha Israel ambayo imekuwa ikifanya mauaji dhidi ya raia katika Ukanda wa Gaza huko Palestina.
-
Intelijensia ya Marekani: HAMAS itaendelea kutoa changamoto kwa Israel kwa "miaka kadhaa"
Mar 12, 2024 23:16Ripoti ya tathmini ya kiintelijensia iliyotolewa na Marekani imetilia shaka uwezo wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kuifuta Hamas, harakati hiyo ya muqawama ya Palestina huenda ikatoa changamoto "ya muda mrefu" kwa miaka kadhaa kwa utawala huo ghasibu unaokalia ardhi za Palestina kwa mabavu.
-
Kuendelea himaya ya Marekani kwa Israel; kuongezeka mashahidi wa Kipalestina katika anga ya uhaba wa chakula na dawa
Mar 12, 2024 22:40Kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni katika kivuli cha uungaji mkono wa Marekani kwa utawala huo na kufungwa njia za kufikisha misaada na kuingia chakula na dawa katika Ukanda wa Gaza kumesababisha kuongezeka la idadi ya mashahidi wa Palestina.
-
Watunisia waandamana mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Tunis dhidi ya Israel
Mar 12, 2024 04:11Wananchi wa Tunisia jana waliandamana mbele ya ubalozi wa Marekani huko Tunis mji mkuu wa Tunisia kulaani mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya raia wa Kipalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Iran: Msaada wa kimaonyesho wa US kwa Gaza ni mchezo mchungu wa kuigiza
Mar 11, 2024 08:35Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani kile alichokitaja kuwa onyesho chungu la kipropaganda la Marekani na kueleza kuwa, hatua ya Washington ya kudai kuwapa misaada ya kibinadamu Wapalestina wa Gaza, na wakati huo huo inazuia juhudi za kimataifa za usitishaji vita katika eneo hilo lililozingirwa, ni kichekesho.
-
Kukosolewa propaganda za Marekani kuhusiana na misaada ya kibinadamu
Mar 10, 2024 07:50Akihutubia bunge la Marekani siku ya Alkhamisi, Rais Joe Biden alisema ameliamuru jeshi la nchi hiyo kuweka bandari kwenye pwani ya Gaza katika Bahari ya Mediterania.
-
Wapalestina watano wauawa na misaada wa kudondoshwa kutoka angani, Gaza
Mar 09, 2024 08:19Wapalestina watano wameuawa na vifurushi vya misaada vilivyodondoshwa na ndege za Marekani na washirika wake kwenye Ukanda wa Gaza unaozingirwa na Israel, huku mamlaka ya Gaza ikilishutumu zoezi hilo kuwa ni "propaganda tupu" na sio huduma ya kibinadamu.