Mar 12, 2024 07:41 UTC
  • Watunisia waandamana mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Tunis dhidi ya Israel

Wananchi wa Tunisia jana waliandamana mbele ya ubalozi wa Marekani huko Tunis mji mkuu wa Tunisia kulaani mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya raia wa Kipalestina wa Ukanda wa Gaza.

Katika maandamano hayo, wananchi wa Tunisia wamewataka viongozi wa nchi hiyo kumfukuza balozi wa Marekani nchini Tunisia ili kupinga  uungaji mkono wa nchi hiyo kwa utawala wa Kizayuni.  

Waandamanaji hao ambao walikuwa wamebeba bendera za Palestina, Yemen na Afrika Kusini walipiga nara "Tunatoe mhanga nafsi na roho zetu kwa ajili ya Palestina." 

Wakati huo huo, wanawake wa Morocco wamefanya maandamano makubwa katika miji mbalimbali ya nchi hiyo kwa lengo la kuwaunga mkono wenzao wa Palestina hususan wanawake wa Ukanda wa Gaza. 

Maandamano ya wananchi wa Tunisia dhidi ya uungaji mkono wa Marekani kwa utawala wa Kizayuni 

Jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina zimechochea hisia za walimwengu, ambapo wananchi, serikali na taasisi mbalimbali za kimataifa duniani wametoa wito wa kuwatetea watu wanaodhulumiwa wa Palestina dhidi ya mashambulizi ya kikatili ya Israel.

Tags