-
Watu 12 wauawa katika hujuma za wanamgambo wa ADF nchini DRC
Jan 26, 2022 12:07Watu wasiopungua 12 wameuawa katika mkoa wa Ituri, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kufuatia mashambulio ya waasi wa Uganda wa ADF.
-
Makumi ya watu wauawa katika mapigano ya kikabila Sudan Kusini
Jan 25, 2022 07:59Watu wasiopungua 30 wameuawa huku wengine wengi wakijeruhiwa katika mapigano ya kikabila nchini Sudan Kusini.
-
Saudia yaua raia wa Yemen, ikiwemo familia nzima, katika hujuma dhidi ya Sana'a
Jan 19, 2022 03:02Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Yemen amesema muungano wa kivita wa Saudi Arabia umetekeleza mashambulizi dhidi ya mji mkuu wa Yemen, Sana'a, ambapo raia 20, ikiwemo familia moja wameuawa.
-
Zaidi ya wasanii 20 wasusia Tamasha la Sydney, wanapinga ufadhili wa Israel
Jan 08, 2022 02:49Zaidi ya wasanii 20 hadi sasa yamejiondoa kwenye Tamasha la Sydney 2022 kupinga mchango wa kifedha uliotolewa na ubalozi wa utawala haramu wa Israel nchini Australia kwa moja ya maonyesho ya tamasha hilo.
-
Watoto 2 ni kati ya wakimbizi 3 wa Eritrea waliouawa huko Tigray
Jan 07, 2022 15:27Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, raia watatu wa Eritrea wakiwemo watoto wawili wameuawa katika shambulio la anga lililoilenga kambi ya wakimbizi katika eneo la Tigray lililoathiriwa na mapigano huko kaskazini mwa Ethiopia.
-
Wito wa Wahindu wa kutekelezwa mauaji ya kimbari dhidi ya Waislamu waibua hasira
Dec 25, 2021 04:32Video zinazowaonyesha viongozi wa kidini wa Kihindu nchini India wakitoa wito wa mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu zimezua hasira na wito madai ya kuchukuliwa hatua dhidi ya wahusika.
-
Polisi ya Uturuki yazima njama ya mauaji dhidi ya Rais Erdogan
Dec 05, 2021 07:16Vyombo vya habari vya Uturuki vimeripoti kuwa, polisi ya nchi hiyo imegundua na kulipua bomu lililokuwa limetegwa eneo ambako Rais wa nchi hiyo, Recep Tayyip Erdoğan, alipangiwa kuhutubia wananchi huko kusini mwa Uturuki.
-
Emmanuel Macron ashutumiwa kwa kujaribu 'kumsafisha' Mohammed bin Salman
Dec 05, 2021 03:03Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamekosoa mkutano wa Rais Emmanuel Macron na Ufaransa na mriti wa ufalme wa Saudia Mohammed bin Salman jana Jumamosi huko Riyadh yakisisitiza kuwa mkutano huo una lengo la kumsafisha mrithi huo wa ufalme wa Saudia aliyeamuru kuuawa kigaidi mwandishi habari jamal Khashoggi.
-
Le Monde: Sudan inaishi siku zake mbaya zaidi za umwagaji damu tangu baada ya mapinduzi
Nov 19, 2021 02:58Gazeti la Le Monde la Ufaransa limeripoti kuwa Sudan inaishi katika kipindi kibaya zaidi cha ukandamizaji na mauaji ya raia tangu baada ya mapinduzi ya kijeshi ya tarehe 25 Oktoba mwaka huu yaliyoindoa madarakani serikali ya kipindi cha mpito.
-
Familia ya Waafghani waliouawa na Marekani: Kuungama hakutoshi, wahusika wachukuliwe hatua
Sep 19, 2021 16:33Familia ya raia kumi wa Afghanistan waliouawa katika shambulizi la ndege isiyo na rubani ya jeshi la Marekani mjini Kabul imekataa hatua ya serikali ya Washington ya kuungama na kuomba radhi kutokana mauajii hayo.