Pars Today
Waziri wa Mambo ya Nje ya Misri amekosoa hatua ya utawala haramu wa Israel ya kupora na kuzuia kuingizwa na kusambazwa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza, kupitia kivuko cha Rafah.
Leo ni Ijumaa tarehe 7 Mfunguo Tatu Dhul-Hijja 1445 Hijria mwafaka na tarehe 14 Juni 2024 Miladia.
Leo ni Jumatano tarehe 5 Mfunguo Tatu Dhul-Hija 1445 Hijria ambayo inasadifiana na tarehe 12 Juni 2024 Miladia.
Katika mazungumzo ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitizia ulazima wa kuunganishwa nguvu za nchi za Waislamu katika kukabiliana na utawala wa Kizayuni.
Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametuma salamu za rambirambi kwa familia za shahidi Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wenzake aliokuwa amefuatana nao na kutoa mkono wa pole kwa serikali na wananchi wa Iran.
Mwakilishi wa Misri katika Umoja wa Matiafa amesema kuwa hali ya mambo katika Ukanda wa Gaza imefikia katika ukingo wa njaa.
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Misri imetangaza kuungana na mashtaka ya Afrika Kusini dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel unaofanya mauaji katika Ukanda wa Gaza.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri amesema kuwa jamii ya kimataifa imeshindwa kuzuia mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza. Sameh Shukry ameeleza haya katika mazungumzo na Mjumbe Maalumu wa Ufaransa katika Masuala ya Lebanon.
Ujumbe wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) umeondoka Cairo, mji mkuu wa Misri ili kufanya mashauriano zaidi kuhusu pendekezo jipya lililotolewa kwa ajili ya kubadilishana mateka.
Mkutano wa pande tatu wa mawaziri wa mambo ya nje wa Misri, Jordan na Ufaransa ulifanyika Jumamosi Cairo, mji mkuu wa Misri, kuhusiana na matukio ya hivi karibuni katika vita vya Gaza na mashauriano ya kusitisha mapigano hayo.