Pars Today
Wanasiasa wa kambi ya upinzani nchini Misri wamewataka wananchi wa nchi hiyo kususia uchaguzi ujao wa rais.
Wakili wa mkuu wa zamani wa jeshi la Misri ambaye ametangaza kuchuana na Rais Abdul Fattah el Sisi katika uchaguzi ujao wa rais nchini humo amesema kuwa, mteja wake emepelekwa katika jela ya kijeshi.
Harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri imetahadharisha kuhusu hatua ya serikali ya nchi hiyo inayoongozwa na Rais Abdel Fatah al Sisi ya kuwashinikiza wapinzani wa serikali na taathira zake mbaya za kisiasa.
Mpinzani wa Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri katika kinyang'anyiro cha uchaguzi ujao wa Rais ametangaza kujitoa katika mbio hizo hatua ambayo inamsafishia njia Rais wa sasa wa nchi hiyo kutetea kiti chake.
Waziri Mkuu wa Ethiopia amekataa pendekezo la Misri la kuitaka Benki ya Dunia kuwa mpatanishi katika mgogoro wa ujenzi wa bwawa unaofanywa na serikali ya Addis Ababa juu ya Mto Nile.
Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri ametangaza kuwa atawania muhula wa pili wa urais katika uchaguzi wa mwezi Machi ambapo anatazamiwa kushinda.
Washiriki wa mkutano wa kimataifa wa kuunga mkono Quds uliofanyika katika Chuo Kikuu cha al-Azhar huko Cairo Misri umesisitiza umuhimu wa kutangazwa Baytul-Muqaddas kuwa mji mkuu wa milele wa Palestina.
Mkuu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Baraza la Shirikisho la Russia amesema kuwa, serikali ya Moscow, haina nia yoyote ya kuanzisha kambi za kijeshi katika nchi za Misri na Libya.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amesema kuwa, lau ingelitaka, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ingeliweza kutumia tofauti zake za kisiasa na Doha kuwatesa kwa njaa wananchi wa Qatar, lakini kamwe haikufanya hivyo.
Bunge la Misri limetangaza kurefusha muda wa hali ya hatari nchini humo kwa miezi mitatu mingine ambao ulianza kutekelezwa mwezi Aprili mwaka jana baada ya kujiri mashambulizi makubwa katika makanisa ya Wakristo wa Kikopti nchini humo.