-
"Mantiki ya Muqawama ya IRGC ndiyo njia pekee ya kuwaokoa Waislamu"
Mar 11, 2025 04:39Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Meja Jenerali Hossein Salami amesema mantiki ya Muqawama ya SEPAH ndiyo njia pekee ya kuwaokoa Waislamu mkabala wa kutawaliwa na maadui.
-
Spika Qalibaf: Namna Hizbullah ilivyoonyesha nguvu zake imedhihirika kuwa Muqawama hauondosheki
Feb 25, 2025 10:39Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema, kutokana na jinsi Hizbullah ilivyoonyesha nguvu na uwezo wake, imemdhihirikia wazi kila mtu kwamba maadui hawawezi kuuondoa Muqawama au kuuweka kando ya ulingo wa kisiasa na kiusalama wa Lebanon kutokana na uungaji mkono wa wananchi ilionao.
-
HAMAS: Kuwa na silaha ni haki ya kisheria ya Muqawama na kuachana nazo ni jambo lisilowezekana
Feb 25, 2025 09:46Hazem Qassem, msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS ameashiria matamshi yaliyonasibishwa na kiongozi mwandamizi wa harakati hiyo Musa Abu Marzouk na kusisitiza kwamba: "Hamas inaendelea kutumia silaha za Muqawama kama haki halali na ya kisheria na haitalegeza msimamo juu ya suala hilo".
-
Iran kuwakilishwa na Spika wa Bunge, Waziri wa Mambo ya Nje katika mazishi ya Shahidi Nasrallah
Feb 23, 2025 03:47Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) Mohammad Baqer Qalibaf na Waziri wa Mambo ya Nje Abbas Araghchi leo wanaelekea Beirut kushiriki katika hafla ya mazishi ya kiongozi wa Hizbullah aliyeuawa shahidi, Sayyed Hassan Nasrallah, pamoja na mkuu wa Baraza la Utendaji la Hizbullah, Shahidi Sayyid Hashim Safieddine.
-
Salami: Njama za US, Israel kudhuru Muqawama zimegonga mwamba
Feb 21, 2025 07:36Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC), Meja Jenerali Hossein Salami amesema, hakuna shaka kwamba juhudi za Marekani na utawala wa Kizayuni za kujaribu kuudhuru mrengo wa Muqawama zitafeli na kugonga mwamba.
-
Iran: Tunapinga mpango wowote wa kufukuzwa Wapalestina Gaza
Feb 19, 2025 12:07Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran), Mohammad Bagher Ghalibaf amesema kuwa Tehran inapinga vikali na kulaani mpango wowote unaokusudia kuwafurusha Wapalestina katika ardhi zao.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Mpango wa kijinga wa Marekani kuhusu Gaza hautafika popote
Feb 18, 2025 15:15Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, akiwapongeza wapiganaji wa Muqawama kwa ushindi wao katika Ukanda wa Gaza, amesisitiza kwamba kazi kubwa ya viongozi na wapiganaji wa Muqawama wa Palestina ipo katika "umoja na mshikamano" na "kusimama imara" dhidi ya adui, kuendesha mchakato mgumu wa mazungumzo, pamoja na uvumilivu na ustahimilivu wa wananchi, ambavyo vimeinua heshima ya Muqawama katika eneo.
-
Wapalestina wa Ghaza: Trump ni majinuni, hajui chochote kuhusu ardhi yake mtu, sharafu wala Palestina
Feb 06, 2025 03:26Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza wameubeza na kuukebehi mpango wa Rais wa Marekani wa kuwataka wahame moja kwa moja katika ardhi yao hiyo ya Palestina ili kupisha ujenzi wa kuigeuza Ghaza eneo la burudani watakaloishi ndani yake watu wa kila pembe ya dunia.
-
Mkuu wa Hizbullah: Lebanon haitasahau msaada wa Iran, Iraq wakati wa vita vya Israel
Jan 28, 2025 08:03Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, watu wa Lebanon hawatasahau uungaji mkono na msaada mkubwa waliopewa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Iraq wakati wa mashambulizi makali ya anga na nchi kavu ya Israel dhidi ya nchi yao.
-
Hizbullah: Irada ya Walebanon, ndiyo silaha kubwa zaidi ya Muqawama
Jan 27, 2025 12:30Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon imepongeza hatua ya kurejea maelfu kwa maelfu ya watu katika miji yao ambayo ingali inakaliwa kwa mabavu kusini mwa Lebanon, huku wakipuuzilia mbali vitisho vya jeshi la Israel, ikisema nia yao isiyo na kikomo na moyo wao usioweza kutetereshwa, ndiyo silaha kali zaidi za mrengo wa Muqawama.