"Mantiki ya Muqawama ya IRGC ndiyo njia pekee ya kuwaokoa Waislamu"
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Meja Jenerali Hossein Salami amesema mantiki ya Muqawama ya SEPAH ndiyo njia pekee ya kuwaokoa Waislamu mkabala wa kutawaliwa na maadui.
Akizungumza katika Marasimu ya Tatu ya Qur'ani jana Jumatatu hapa mjini Tehran, Mkuu wa IRGC amesisitiza kuwa, mantiki ya Muqawama wanayofungamana nayo walinzi wa Iran ndiyo pekee inayoweza kuwaokoa Waislamu kutoka katika utumwa na kutawaliwa na maadui.
"Uvumilivu ni dhihirisho wazi la subira, uaminifu, na kutafuta kimbilio mkabala wa magumu," amesisitiza Kamanda Salami na kuongeza: Waumini walipoingia kwenye uwanja wa vita wakiwa na imani, subira, na uaminifu, mmoja wao angelishinda dhidi ya maadui kumi, na ikiwa waumini wataonyesha udhaifu, uwiano huu ungebadilika.
Salami ameeleza bayana kuwa, wapiganaji wa Yemen ni mfano wa wazi wa dalili hizi tukufu za Mwenyezi Mungu; walisimama dhidi ya adui mwenye kiburi na wala hawakuogopa.
"Watu wa Yemen, Iraq, Hizbullah ya Lebanon, na ndugu wa Palestina wameelewa ukweli huu vyema kwenye medani ya vita," Salami alisema, akibainisha, "Pia tumegusia ukweli huu na ukweli wa Kimaanawi kwa miaka mingi kwenye medani za jihadi. Njia yetu ya uokovu ni kukimbilia Quran Tukufu."
Kitabu hiki kitakatifu ndiyo dawa ya kweli ya furaha ya mwanadamu, inayowaongoza kutoka kwenye giza la ujinga hadi kwenye nuru ya maarifa na imani," Meja Jenerali Salami amesisitiza.