Utafiti: Mlipuko wa Ebola Kongo ulianza miezi kadhaa kabla ya kugunduliwa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i140332-utafiti_mlipuko_wa_ebola_kongo_ulianza_miezi_kadhaa_kabla_ya_kugunduliwa
Utafiti: Mlipuko wa Ebola Kongo ulianza miezi kadhaa kabla ya kugunduliwa
(last modified 2026-08-01T11:26:02+00:00 )
Aug 01, 2026 11:24 UTC
  • Mlipuko wa Ebola Kongo ulianza miezi kadhaa kabla ya kugunduliwa
    Mlipuko wa Ebola Kongo ulianza miezi kadhaa kabla ya kugunduliwa

Utafiti: Mlipuko wa Ebola Kongo ulianza miezi kadhaa kabla ya kugunduliwa

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watafiti waliwahoji takriban watu 100 ndani na nje ya mji wa Mongbwalu wakiwemo walezi, viongozi wa jamii, manusura, ndugu wa wahanga, watengenezaji wa majeneza na walinzi wa makaburi.

"Ripoti hiyo ya jarida la Science iliyochapishwa jana Julai 30 mwaka huu, ilihitimisha kuwa mlipuko huo ulianza mwezi Januari au labda hata mapema zaidi katika maeneo ya pembezoni mwa mji wa Mongbwalu katika jimbo la Ituri.

Upo uwezekano kwamba mgonjwa aliyekuwa akitafuta matibabu alipeleka maambuzi mjini kutoka eneo la vijijini," imeeleza ripoti hiyo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa: Pale mamlaka za afya jijini Kinshasa zilipotambua ugonjwa huo kuwa ni homa ya Ebola, tayari kulikuwa na "mlipuko mkubwa na ulioenea kwa kiasi kikubwa."

Maafisa wa afya wa Kongo wameeleza kuwa mlipuko wa hivi karibuni wa Ebola nchini umetajwa kuwa mlipuko wa pili kwa ukubwa duniani kwa idadi ya maambukizi yaliyorekodiwa, huku zaidi ya visa 3,530 na vifo 1,556 vikirekodiwa tangu mlipuko huo utangazwe katikati ya mwezi wa Mei.

Wakati huo huo katikati ya mwezi Januari na tarehe 15 Mei mwaka huu watafiti waligundua zaidi ya 500 walioshukiwa kuambukizwa ugonjwa wa Ebola.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mnyororo mmoja wa maambukizi ulianza kwa mwanamke mwenye umri wa miaka 50 aliyefariki dunia tarehe 25 Januari baada ya kutapika damu. Mama yake pia alifariki dunia siku sita baadaye, huku mumewe akiugua lakini akapona.