-
Qatar: Palestina ni kadhia muhimu zaidi ya nchi za Kiislamu na Kiarabu
Sep 12, 2019 07:16Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amelaani hatua ya Wazayuni kukiuka haki za taifa la Palestina na kusema: "Palestina ni kipaumbele cha kwanza kwa nchi za Kiislamu na Kiarabu."
-
Malengo ya safari ya waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni huko Al Khalil
Sep 06, 2019 01:34Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Utawala wa Kizayuni wa Israel Septemba Nne, kwa mara ya kwanza alifika katika mji wa Al Khalil (Hebron) katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kisha akaingia katika msikiti maarufu wa Masjid Ibrahimi katika mji huo. Kabla ya safari hiyo ya Netanyahu, rais wa utawala wa Kizayuni Reuven Rivlin naye pia alifika katika mji wa Al Khalil na kutembelea Masjid Ibrahimi.
-
Makumi ya Wapalestina wajeruhiwa kwa risasi katika maandamano ya "Haki ya Kurejea"
Aug 31, 2019 03:12Makumi ya Wapalestina wamejeruhiwa kwa risasi katika Ijumaa ya 72 ya maandamano ya 'Haki ya Kurejea' yaliyofanyika kwa kaulimbiu ya "Utiifu kwa Mashahidi.
-
Mahmoud Abbas: Marekani haisaidii juhudi za kurejesha amani Mashariki ya Kati
Aug 30, 2019 22:14Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema kuwa Marekani haisaidii juhudi za kurejesha amani na usalama katika eneo la Mashariki ya Kati.
-
Makampuni ya Imarati yanunua ardhi za mji wa Quds kwa ajili ya Wazayuni
Aug 29, 2019 03:22Naibu Mwenyekiti wa Harakati ya Kiislamu ya Palestina amesema kuwa makampuni ya Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) yananunua ardhi huko Quds na kisha kukabidhi umiliki wa ardhi hizo kwa Waisraeli.
-
Arab League: Uamuzi wa Marekani wa kulifuta jina la Palestina ni kitendo cha "uadui"
Aug 28, 2019 22:07Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) imesema, uamuzi mpya uliochukuliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani wa kulifuta jina la Palestina katika orodha ya maeneo ya Magharibi ya Asia ni kitendo cha "uadui".
-
Marekani yafuta jina la Palestina katika orodha ya nchi za dunia
Aug 26, 2019 08:25Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imechukua hatua isiyo ya kawaida kwa kufuta jina la Palestina katika orodha ya nchi na maeneo mbalimbali ya dunia.
-
OIC: Baitul Muqaddas (Jerusalem) ni mji mkuu wa Palestina
Aug 22, 2019 07:41Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imesisitiza kuwa: Baitul Muqaddas utabakia daima kuwa mji mkuu wa Palestina.
-
Wabunge Waislamu wa Marekani watamka hadharani kuwa iko siku ya karibu wataizuru Palestina ikiwa huru
Aug 18, 2019 22:13Wabunge wawili Waislamu katika Kongresi ya Marekani, ambao wamezuiwa kutembelea ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu wametangaza hadharani kuwa, iko siku ya karibu mno, wataitembelea Palestina ikiwa huru.
-
Utawala wa Kizayuni unashirikiana na Trump katika hatua dhidi ya wabunge Waislamu katika Kongresi ya Marekani
Aug 17, 2019 03:20Wizara ya Mambo ya Nje ya Utawala wa Kizayuni wa Israel imetangaza kuwa haitawaruhusu wajumbe wawili wa Bunge la Marekani, Kongresi, kuingia katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.