-
Walowezi wa Kiyahudi wavamia Msikiti wa al Aqsa mara tatu siku ya Idi, wajeruhi makumi ya Waislamu
Aug 11, 2019 22:14Walowezii zaidi ya 1700 wa Kiyahudi jana walivamia Msikiti wa al Aqsa mara tatu katika siku ya Idul Adh'ha na kuwajeruhi makumi ya Waislamu waliokwenda eneo hilo takatifu kwa ajili ya kufanya ibada.
-
Saeb Erakat: Mamlaka ya Ndani ya Palestina inafuatilia kuundwa nchi ya Palestina
Aug 05, 2019 03:45Katibu wa kamati ya utendaji ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) ametangaza kuwa, mkakati wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ni kuhitimishwa uvamizi na ukaliaji mabavu wa Wazayuni na kuundwa nchi ya Palestina.
-
Waziri Mkuu wa Palestina: Bila mfumo wa madola mawili, Israel itafikwa na kifo cha kidemografia
Jul 31, 2019 08:21Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mohammad Shtayyeh amesema, utawala wa Kizayuni wa Israel utakabiliwa na "kifo cha kidemografia" ikiwa utakataa kuunga mkono suluhisho la kuwepo madola mawili, kwa ajili ya kutatua mgogoro wa miongo kadhaa baina yake na Wapalestina.
-
Russia yakosoa kitendo cha Marekani kukwamisha kupasishwa tamko la kulaani kubomolewa nyumba za Wapalestina
Jul 30, 2019 06:28Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imekitaja kitendo cha Marekani cha kuzuia kupasishwa taarifa inayolaani kubomolewa nyumba za raia wa Palestina katika mji wa Quds kuwa ni ishara nyingine ya upuuzaji wa Washington wa sheria za kimataifa.
-
Mufti wa Syria: Waislamu waungane katika suala la Palestina
Jul 29, 2019 22:27Mufti Mkuu wa Syria amewahimiza Waislamu washikamane na kuwa kitu kimoja dhidi ya njama zinazopikwa na maadui dhidi ya kadhia ya Palestina.
-
Baraza la Taifa la Palestina lamuunga mkono Mahmoud Abbas kwa kusitisha utekelezaji wa makubaliano na Israel
Jul 27, 2019 23:36Baraza la Taifa la Palestina limetangaza kuwa, kusitishwa utekelezaji wa hati za makubaliano yaliyofikiwa kati ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina na Israel ni mwanzo wa awamu mpya ya makabiliano ya pande zote na Wazayuni maghasibu.
-
Katibu Mkuu wa UN: Ubomoaji nyumba za Wapalestina si halali kisheria
Jul 26, 2019 02:56Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema, anatiwa wasiwasi na ubomoaji nyumba za Wapalestina unaofanywa na utawala wa Kizayuni na kusisitiza kuwa, sera za Israel za kuharibu na kuteketeza mali za Wapalestina haziendani na sheria za kimataifa.
-
Walowezi wa Kizayuni wavamia tena Msikiti Mtakatifu wa al-Aqswa
Jul 25, 2019 21:04Makumi ya walowezi wa Kizayuni wameuvamia tena Msikiti wa al-Aqswa huko Palestina wakisaidiwa na askari wa jeshi la utawala haramu wa Israel na kuuvunjia heshima msikiti huo mtakatifu na kibla cha kwanza cha Waislamu.
-
Kubomolewa nyumba za Wapalestina baada ya vita; jinai zisizo na kikomo za Israel
Jul 23, 2019 23:26Utawala wa Kizayuni wa Israel baada ya kushindwa katika vita vilivyodumu kwa muda wa siku mbili tu, hivi sasa umeanzisha duru mpya ya jinai zake dhidi ya Wapalestina kwa kubomoa nyumba za wananchi hao madhulumu.
-
Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina yalaani kuharibiwa nyumba za Wapalestina mjini Quds
Jul 22, 2019 08:59Wizara ya Mambo ya Nje ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imelaani kitendo cha utawala haramu wa Kizayuni wa Israel cha kubomoa nyumba za Wapalestina katika eneo la Sur Baher katika mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu.