-
Mwanamfalme wa Qatar: Saudia iliyoiuza al-Aqsa kwa adui, haina haki ya kusimamia al-Kaabah
May 19, 2018 14:05Mjukuu wa mwasisi wa taifa la Qatar sambamba na kukosoa vikali mienendo ya Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud wa Saudi Arabia kwa kuitumikia Marekani na utawala wa Kizayuni, amesema kuwa mtu ambaye ameiuza Masjidul-Aqsa kwa adui wa Uislamu, hafai kuwa msimamizi wa nyumba ya Mwenyezi Mungu ya al-Kaabah.
-
Qatar kuendelea kuisaidia Somalia huku mgogoro na Imarati ukitokota
May 15, 2018 13:44Qatar imeahidi kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya Somalia za kurejesha uthabiti na uhuru wa kujitawala huku mgogoro kati ya nchi hiyo ya Pembe ya Afrika na Umoja wa Falme za Kiarabu ukiendelea kutokota.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar: mzingiro dhidi ya Qatar ni kwa ajili ya kuficha matatizo ya ndani Saudia
May 13, 2018 15:42Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amesema kuwa sababu iliyopelekea nchi yake kuwekewa mzingiro ni kutaka kuficha matatizo ya matukio ya ndani ya Saudi Arabia, Imarati na Bahrain.
-
Saudia: Sharti serikali ya Qatar itume vikosi Syria ili isipinduliwe
Apr 25, 2018 07:27Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia amesema iwapo serikali ya Qatar inataka isiondolewe madarakani na iendelee kudhaminiwa usalama na Marekani, sharti itume wanajeshi wake nchini Syria.
-
Nchi zinazoizingira Qatar zakariri madai yao kwa Doha kama sharti la kufungua upya mahusiano
Apr 13, 2018 07:23Kwa mara nyingine nchi nne za Kiarabu zainazoizingira Qatar ambazo ni Saudi Arabia, Bahrain, Imarati na Misri, zimekariri masharti yao 13 kwa serikali ya Doha kama njia ya kufungua upya uhusiano wao na nchi hiyo.
-
Marekani yaiuzia Qatar makombora 5000 huku mgogoro na Saudia ukitokota
Apr 11, 2018 04:35Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imetangza idhini ya kuiuzia Qatar makombora 5000 yenye thamani ya dola milioni 300 huku mgogoro baina ya nchi hiyo ndogo na Saudia ukizidi kutokota.
-
Saudia inapanga kuigeuza Qatar kisiwa na jalala la takataka za nyuklia
Apr 10, 2018 16:55Saudi Arabia inapanga kuanzisha mradi wa ujenzi wa mfereji kwenye mpaka wake wa pamoja wa ardhini na Qatar ambao utaigeuza nchi hiyo ndogo ya Kiarabu katika Ghuba ya Uajemi kuwa kisiwa.
-
Malengo ya safari ya Amiri wa Qatar nchini Russia
Mar 28, 2018 10:28Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, Amiri wa Qatar amefanya safari nchini Russia na kukutana na Rais Vladmir Putin wa nchi hiyo ambapo wamezungumzia masuala mbalimbali.
-
Qatar: Imarati imetutaka kuachana na maandalizi ya Kombe la Dunia 2022 ili iache kutuzingira
Mar 24, 2018 14:46Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Qatar amefichua kwamba, nchi nne zinazoizingira nchi hiyo zikiongozwa na Saudi Arabia, zimetoa sharti zito kwa Doha kwamba, inatakiwa kuchagua moja ya mambo mawili, ima kuachana na maandalizi ya michuano ya kombe la dunia 2022, au kuendelea kuzingirwa na nchi hizo.
-
Bara la Afrika ni medani ya duru mpya ya malumbano baina ya Qatar na kundi la Kiarabu la 3+1
Mar 15, 2018 07:16Ushahidi unaonyesha kuwa, bara la Afrika sasa limegeuka na kuwa medani mpya ya mashindano ya kuwania ushawishi katika mgogoro unaonedelea kutokota baina ya Qatar na madola ya Kiarabu ya 3+1.