Pars Today
Afisa wa ngazi za juu wa usalama katika Umoja wa Falme za Kiarabu amesema mgogoro uliopo kati ya Doha na nchi kadhaa za Kiarabu zikiongozwa na Saudi Arabia utapatiwa ufumbuzi iwapo Qatar itaachana na azma yake ya kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2022.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran leo subuhi ameondoka Tehran na kuelekea ziarani mjini Muscat Oman kwa ajili ya mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo na Qatar.
Serikali kuu ya Somalia imekosoa vikali hatua ya eneo lenye mamlaka ya ndani la Galmudug kutangaza kuwa linaziunga mkono Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu katika mgogoro wa nchi za Kiarabu.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri amesema kuwa nchi nne zilizoiwekea vikwazo Qatar ziko tayari kutatua mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo.
Mwanamfalme, Abdullah bin Ali Aal Thani kutoka familia ya kifalme ya Qatar amekosoa siasa za Amir wa nchi hiyo, Sheikh Tamim bin Hamad Aal Thani na kumtaka aitishie kikao cha kitaifa cha kujadili mgogoro wa nchi hiyo.
Kamanda wa gadi ya ulinzi wa fukweni ya Bahrain amesema kuwa, vikosi vya ulinzi wa fukweni vya Qatar vimekamata boti tatu za nchi hiyo katika kipindi cha siku mbili zilizopita.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan ameeleza kuwepo mazungumzo kati ya Sudan na Qatar kwa ajili ya kupanua zaidi mahusiano ya pande mbili.
Katika hali ambayo kwa mara nyingine moto wa mgogoro kati ya Qatar na Saudia umeibuka, wawakilishi wa nchi mbili katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) kwa mara nyingine wameshambuliana kwa maneno kuhusiana na nasafi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika eneo la Mashariki ya Kati.
Maafisa usalama nchini Saudi Arabia wamewatia mbaroni mashekhe wawili wa nchi hiyo kwa kosa la eti kufadhiliwa kifedha na Qatar katika harakati zao za kidini.
Gazeti la New York Times la nchini Marekani limesema kuwa, rais wa nchi hiyo, Donald Trump ameshindwa kutatua mgogoro wa Qatar na nchi nne za Kiarabu zinazoongozwa na Saudia.