Sep 09, 2017 08:03
Licha ya kuwa kumeanza duru mpya ya juhudi za upatanishi wa kuutatua mgogoro unaofukuta kati ya Qatar na kundi la 3+1, lakini Mohammed bin Abdulrahman Al Thani, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Qatar kwa mara nyingine tena amesisitiza kuwa, nchi yake itakaa katika meza ya mazungumzo pale tu mamlaka ya kujitawala Doha yatakapoheshimiwa na kutotiwa dosari.