-
Qatar yakadhibisha madai mapya ya Saudi Arabia
Jul 26, 2017 22:53Mkurugenzi wa Ofisi ya Mawasiliano ya serikali ya Qatar ameyataja madai mapya ya nchi nne za Kiarabu zilizoiwekea Doha vikwazo kuwa ni ya uwongo na yenye kukatisha tamaa.
-
Nchi nne za Kiarabu zashadidisha vikwazo vyao dhidi ya Qatar
Jul 25, 2017 09:46Nchi nne za Kiarabu zilizovunja uhusiano wao wa kidiplomasia na Qatar na kuiwekea vikwazo nchi hiyo ya Kiarabu leo zimetoa orodha mpya ya majina ya taasisi na shakhsia zinaodai kuwa wana mfungamano na makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na Qatar.
-
London yakaribisha juhudi za Doha za kupunguza mivutano kati yake na nchi za Kiarabu
Jul 24, 2017 02:47Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza amekaribisha juhudi za serikali ya Qatar za kupunguza mivutano kati yake na nchi za Kiarabu za eneo la Ghuba ya Uajemi.
-
Imarati na Saudia zakataa wito wa Qatar wa mazungumzo
Jul 23, 2017 09:37Umoja wa Falme za Kiarabu umekataa wito uliotolewa hivi karibuni na Amir wa Qatar, Sheikh Tamin bin Hamad al-Thani, wa kufanyika mazungumzo ya kuupatia ufumbuzi mgogoro uliopo, na kusisitiza kuwa Doha sharti ibadili sera zake kabla ya kufanyika jitihada zozote za kuiondolea vikwazo nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi, iivyowekewa na Saudia na wapambe wake.
-
Qatar: Tangu awali tulipinga muungano wa Saudia wa kuishambulia Yemen
Jul 19, 2017 09:50Waziri wa Ulinzi wa Qatar amesema kuwa, tangu awali Doha ilipinga muungano unaoongozwa na Saudia katika kuishambulia kijeshi Yemen, kwani iliamini utatuzi wa mgogoro huo haukuwa wa kijeshi.
-
Imarati: Juhudi za upatanishi wa Kuwait katika mgogoro wa nchi za Kiarabu zitaambulia patupu
Jul 18, 2017 21:57Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa serikali ya Imarati, Anwar Mohammed Qarqash amesema kuwa, juhudi za upatanishi wa Kuwait kwa ajili ya kutafuta utatuzi wa mgogoro wa nchi za Kiarabu, zitaambulia patupu iwapo Qatar haitabadilisha siasa zake.
-
Qatar kuishtaki Imarat kwa kuhusika na udukuzi
Jul 18, 2017 10:44Serikali ya Qatar imeeleza kusikitishwa sana na hatua ya Imarat ya kudukua mitandao ya intaneti ya serikali ya Doha, suala ambalo limeibuka mgogoro wa sasa kati ya nchi hizo mbili na kusisitiza kuwa, Doha itawafungulia mashtaka wahusika wa uhalifu huo.
-
Kuzidi kutokota mgogoro ndani ya Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi
Jul 17, 2017 05:28Baada ya Rex Tillerson, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kushindwa kupatanisha mgogoro wa nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi ulioanzishwa na Saudi Arabia dhidi ya Qatar, maafisa wa kijasusi wa Marekani wametangaza kuwa, Umoja wa Falme za Kiarabu yaani Imarati ndiyo iliyodukua mitandao ya Intaneti ya Qatar na kuzua mgogoro uliopo hivi sasa.
-
Saudia yaichochea FIFA iipokonye Qatar uwenyeji wa Kombe la Dunia 2022
Jul 16, 2017 02:31Saudi Arabia inaziongoza nchi kadhaa za Kiarabu katika kulishinikiza Shirikisho la Soka Duniani kuipokonya Qatar haki ya kuandaa Kombe la Dunia mwaka 2022 kwa madai kuwa nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi inaunga mkono ugaidi.
-
Qatar: Ugaidi wa kisiasa ndio kikwazo cha vita dhidi ya ugaidi
Jul 15, 2017 23:45Serikali ya Qatar imetangaza kuwa, ugaidi wa kisiasa na kifikra wa baadhi ya nchi za eneo la Mashariki ya Kati ndio kikwazo kikuu hii leo katika vita dhidi ya ugaidi.