-
Mfalme wa Morocco aagiza kupelekwa bidhaa za chakula nchini Qatar
Jun 13, 2017 02:46Mfalme wa Morocco ameagiza kutumwa bidhaa za chakula huko Qatar.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar: Mazingira kwa ajili ya mazungumzo bado hayajaandaliwa
Jun 12, 2017 21:56Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar ameashiria akiwa mjini London kuhusu kuendelea jitihada za upatanishi wa Kuwait kwa ajili ya kuupatia ufumbuzi mgogoro uliojitokeza kati ya nchi kadhaa za Kiarabu na nchi yake na kueleza kuwa, mazungumzo ya kidiplomasia ni njia itakayoweza kuupatia ufumbuzi mgogoro uliopo, hata hivyo amesema mazingira ya kufanyika mazungumzo hayo hadi sasa bado hayajaandaliwa.
-
Qatar: Tuliwakaribisha Taliban mjini Doha kwa matakwa ya Marekani
Jun 12, 2017 03:21Afisa wa ngazi za juu wa serikali ya Qatar amesema kuwa, nchi hiyo ililialika kundi la kigaidi la Taliban mjini Doha kutokana na takwa la Marekani ambayo leo, ikiwa pamoja na nchi kadhaa za Kiarabu, inaituhuma Qatar kuwa inaunga mkono makundi yenye misimamo mikali.
-
Saudia yawapiga marufuku raia wa Qatar kuingia Masjid al-Haram
Jun 11, 2017 22:44Mgogoro wa kidiplomasia ulioibuka kati ya Saudi Arabia ikishirikiana na nchi kadhaa za Kiarabu dhidi ya Qatar unaonekana kuchukua sura mpya baada ya watawala wa Aal Saud kuwazuia raia wa Qatar kuingia katika msikiti wa Makka.
-
HAMAS yasifu msimamo wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar
Jun 11, 2017 03:33Msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesifu msimamo wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Muhammad bin Abdulrahman Al Thani wa kusisitiza kwamba Hamas ni harakati halali ya muqawama.
-
AI: Vikwazo vya Saudia na washirika wake dhidi ya Qatar vina taathira mbaya kwa raia wa Ghuba ya Uajemi
Jun 10, 2017 11:26Shirika la Msamaha Duniani (Amnesty International) limetangaza kuwa, hatua iliyochukuliwa na Saudi Arabia na washirika wake ya kuiwekea vikwazo na kuizingira Qatar ni kuchezea maisha ya maelfu ya watu wa Ghuba ya Uajemi.
-
Mgawanyiko katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuhusu mvutano wa Qatar na Saudia
Jun 09, 2017 02:55Misimamo iliyochukuliwa na nchi wanachama katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) kuhusu mivutano inayoendelea baina ya Qatar na Saudi Arabia sambamba na kudhihirisha mgawanyiko na ukosefu wa mshikamano uliopo baina ya nchi za jumuiya hiyo, vilevile umeonesha kuwa, Saudia haiungwi mkono isipokuwa na nchi ndogo na dhaifu.
-
Iran yatenga bandari tatu kuipelekea chakula Qatar
Jun 08, 2017 13:25Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Muhammed bin Abdul Rahman Aal Thani amesema kuwa, Tehran imetenga bandari zake tatu kwa ajili ya kupeleka chakula nchini Qatar.
-
Saudia yaendelea kuzishawishi nchi mbalimbali kukata mahusiano yao na Qatar, mara hii ni Afrika
Jun 08, 2017 10:59Hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu zikiongozwa na Saudia ya katika kukata uhusiano na Qatar imezidi kuwa kubwa huku Riyadh ikiendelea kuzishawishi nchi za Kiafrika kujiunga nayo katika hatua hiyo.
-
Taathira za kieneo za mvutano wa Saudi Arabia na Qatar
Jun 08, 2017 10:58Mvutano katika uhusiano wa Saudi Arabia na Qatar bila shaka utakuwa na taathira kubwa hasi kwa utawala wa Riyadh katika upeo wa kieneo.