Mfalme wa Morocco aagiza kupelekwa bidhaa za chakula nchini Qatar
(last modified Tue, 13 Jun 2017 07:16:41 GMT )
Jun 13, 2017 07:16 UTC
  • Mfalme wa Morocco aagiza kupelekwa bidhaa za chakula nchini Qatar

Mfalme wa Morocco ameagiza kutumwa bidhaa za chakula huko Qatar.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Morocco leo asubuhi imetangaza kuwa nchi hiyo itatuma bidhaa za chakula huko Qatar kwa mujibu wa  mafundisho na sheria za dini na ikiwa ni katika kuonyesha mshikamano kati ya mataifa ya Kiislamu khususan katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani, kufuatia agizo lililotolewa na Mfalme Muhammad wa Sita wa nchi hiyo. 

Mfalme Muhammad wa Sita wa Morocco 

Morocco jana Jumatatu pia ilitangaza kuwa ipo tayari kuwa msuluhishi ili kuupatia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa uliojitokeza kati ya Qatar na Saudia na waitifake wake. Itakumbukwa kuwa, tarehe 6 mwezi huu wa Juni Saudi Arabia, Imarati, Bahrain na Misri zilikata uhusiano wao na Qatar zikidai kuwa, nchi hiyo inaunga mkono ugaidi na makundi yenye misimamo mikali. Hali ya mvutano kati ya nchi hizo na Qatar ilianza siku moja baada ya ziara ya Rais wa Marekani nchini Saudia mwishoni mwa mwezi Mei. 

Rais Donadl Trump wa Marekani ziarani nchini Saudia hivi karibuni 

 

Tags