• Burundi yaadhimisha miaka 57 ya Uhuru + Sauti

    Burundi yaadhimisha miaka 57 ya Uhuru + Sauti

    Jul 01, 2019 16:06

    Leo Jumatano tarehe Mosi Julai 2019, Burundi imesherehekea mwaka wa 57 tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa mkoloni wa Ulaya, Ubelgiji. Rais Pierre Nkurunzinza ametumia fursa hiyo kutangaza hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kuondoa michango ya lazima kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020. Hamida Issa na maelezo zaidi kutoka Bujumbura.

  • Mkuu wa Jeshi la Polisi la Tanzania atembelea eneo walipouliwa Watanzania + Sauti

    Mkuu wa Jeshi la Polisi la Tanzania atembelea eneo walipouliwa Watanzania + Sauti

    Jun 30, 2019 17:10

    Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania (IGP), Simon Sirro amesema imebainika kuwa waliowaua Watanzania 9 kwa kuwapiga risasi na wengine kushambuliwa kwa mapanga ambao ni watu wasiojulikana, walianza chokochoko hizo katika eneo la Kibiti mkoani Pwani baada ya kutimuliwa na na Jeshi la Polisi la Tanzania na wengine wakakimbilia nchi jirani ikiwemo Msumbiji. Maelezo zaidi yamo katika ripoti ya mwandishi wetu wa Dar es Salaam, Ammar Dachi.

  • Mbunge 'Jaguar' anyimwa dhamana nchini Kenya + Sauti

    Mbunge 'Jaguar' anyimwa dhamana nchini Kenya + Sauti

    Jun 28, 2019 17:13

    Mahakama nchini Kenya imemnyima dhamana, Mbunge wa eneobunge la Starehe jijini Nairobi Charles Njagua maarufu kwa jina la ‘Jaguar’ ambaye alikamatwa hivi karibuni na jeshi la polisi la nchi hiyo baada ya kutoa kauli ya kibaguzi dhidi ya Watanzania, Wachina na Waganda wanaoishi katika nchini hiyo mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mbunge huyo atasalia korokoroni hadi pale kesi yake itakaposikilizwa tena. Mwandishi wetu wa Mombasa, Kenya Seifullah Murtadha ana maelezo zaidi......

  • Matukio ya ulimwengu wa Kiislamu na Harith Subeit + Sauti

    Matukio ya ulimwengu wa Kiislamu na Harith Subeit + Sauti

    Jun 28, 2019 15:54

    Kama kawaida, wiki hii pia kuna matukio mengi ya Kiislamu yametokea katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki. Mwandishi wetu wa Zanzibar, Harith Subeit ametukusanyia baadhi ya matukio hayo katika ripoti yake hii ya kila wiki...

  • Polisi wawashikilia watuhumiwa 10 utekaji watu Rwanda + Sauti

    Polisi wawashikilia watuhumiwa 10 utekaji watu Rwanda + Sauti

    Jun 27, 2019 08:59

    Polisi mjini Kigali Rwanda inawashikilia watu kumi na saba wakiwemo Wanyarwanda 15 na Wakenya wawili kwa shutuma za kuwatapeli vijana zaidi ya elfu tatu wakiwaahidi ajira hewa za ujasiriamali. Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi...

  • Mapigano ya kikabila DRC yazitia hofu asasi za kijamii + Sauti

    Mapigano ya kikabila DRC yazitia hofu asasi za kijamii + Sauti

    Jun 20, 2019 02:36

    Asasi za kijamii za jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimekumbwa na wasiwasi baada ya kuzorota hali ya usalama katika mkoa wa Ituri wa kaskazini mwa nchi hiyo kutokana na mapigano ya kikabila yanayoendelea. Mossi Mwasi na maelezo zaidi kutoka Brazzaville.

  • Mahakama ya Katiba DRC yalalamikiwa kwa kutengua uchaguzi wa wabunge wa upinzani + Sauti

    Mahakama ya Katiba DRC yalalamikiwa kwa kutengua uchaguzi wa wabunge wa upinzani + Sauti

    Jun 15, 2019 15:57

    Mabalozi wanne wa nchi za Ulaya huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameilaumu Mahakama ya Katiba ya nchi hiyo kwa kutengua ushindi wa baadhi ya wabunge wa upinzani na kuupatia mrengo unaomuunga mkono Rais Mstaafu, Joseph Kabila. Mossi Mwasi na maelezo zaidi...

  • Bomu la kutegwa ardhini laua askari polisi 10 nchini Kenya + Sauti

    Bomu la kutegwa ardhini laua askari polisi 10 nchini Kenya + Sauti

    Jun 15, 2019 12:41

    Maafisa usalama wasiopungua 10 wameripotiwa kuuawa baada ya gari lao kukanyaga bomu la kutegwa ardhini katika kaunti ya Wajir, katika eneo la kaskazini mashariki mwa Kenya.

  • Wakenya waandamana jijini Nairobi kupinga mradi wa makaa ya mawe Lamu + Sauti

    Wakenya waandamana jijini Nairobi kupinga mradi wa makaa ya mawe Lamu + Sauti

    Jun 12, 2019 16:36

    Mashirika ya kijamii nchini Kenya yakiongozwa na shirika la deCOALonize la kutetea nishati safi wameandaa maandamano makubwa jijini Nairobi kupinga hatua ya serikali ya nchi hiyo kuendelea kufadhili ujenzi wa kiwanda cha kawi ya mawe kisiwani Lamu katika mpaka wa Kenya na Somalia. Omar Elmawi ni mratibu wa kitaifa wa shirika hilo la deCOALonize. Mwandishi wetu wa Mombasa Kenya Seifullah Murtadha amefanya mahojiano naye na hapa anaanza kuelezea kiini cha maandamano hayo

  • Polisi Kenya wamjeruhi vibaya kwa risasi kijana aliyetaka kuingia Ikulu kwa nguvu + Sauti

    Polisi Kenya wamjeruhi vibaya kwa risasi kijana aliyetaka kuingia Ikulu kwa nguvu + Sauti

    Jun 11, 2019 16:38

    Polisi nchini kenya wamempiga risasi na kumjeruhi vibaya jamaa mmoja aliyekua akijaribu kuingia katika ikulu ya rais jijini Nairobi huku akiwa amejihami kwa kisu mkononi. Seifullah Murtadha na maelezo zaidi kutoka Mombasa, Kenya.