-
Watu watano waaga dunia katika mlipuko wa bomu karibu na shule huko Mogadishu
Nov 25, 2021 04:45Watu watano wameuawa na wengine zaidi ya 12 wamejeruhiwa hii leo katika mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari karibu na shule moja katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
-
Mwanahabari mtajika wa redio ya Somalia auawa katika shambulio la kigaidi
Nov 21, 2021 04:49Kundi la kigaidi la al Shabaab lenye mfungamano na mtandao wa al Qaida limehusika katika mlipuko wa bomu uliosababisha kifo cha mwandishi habari mtajika wa redio ya serikali ya Somalia huko Mogadishu.
-
Askari 2 wa Uganda wahukumiwa kifo kwa mauaji ya raia Somalia
Nov 14, 2021 04:46Askari wawili wa Jeshi la Ulinzi la Uganda (UPDF) wanaohudumu kwenye Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) wamehukumiwa kifo, kutokana na mauaji ya raia katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
-
Jeshi la Somalia laangamiza magaidi 9 wa al-Shabaab kusini mwa nchi
Nov 11, 2021 00:44Jeshi la Taifa la Somalia (SNA) limetangaza kuwa limeua magaidi tisa wa kundi la al-Shabaab katika wilaya ya Awdhigle kusini mwa nchi hiyo.
-
Askari wa Uganda kushtakiwa kwenye mahakama ya kijeshi kwa kuua raia Somalia
Oct 23, 2021 04:19Mpango wa Umoja wa Afrika wa kulinda amani nchini Somalia AMISOM umeshauri mahakama ya kijeshi ya Uganda iwafungulie mashtaka askari wa nchi hiyo wanaohudumu katika mpango huo, ambao wamehusishwa na mauaji ya raia nchini Somalia.
-
Alkhamisi tarehe 21 Oktoba 2021
Oct 20, 2021 22:50Leo ni Alkhamisi tarehe 14 Mfunguo Sita Rabiul Awwal 1443 Hijria inayosadifiana na tarehe 21 Oktoba mwaka 2021.
-
Uganda kutuma askari polisi 160 wa kulinda amani Somalia
Oct 15, 2021 00:50Uganda inajiandaa kutuma maafisa wa polisi wapatao 160 nchini Somalia, kwenda kushiriki operesheni za kudumisha amani katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
-
Somalia yatoa wito wa kushirikiana na Kenya baada ya uamuzi wa ICJ
Oct 13, 2021 22:52Rais wa Somalia amesema katika hotuba yake aliyotoa jana Jumatano kwamba, uamuzi uliotolewa siku ya Jumanne na Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ) kuhusu mzozo wa mpaka na Kenya ni fursa kwa nchi mbili hizo kushirikiana.
-
Kenya yapinga uamuzi wa ICJ kuhusu mzozo wa mpaka wa baharini na Somalia
Oct 13, 2021 09:28Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amepinga uamuzi uliotolewa jana Jumanne na Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ), kuhusu mzozo wa muda mrefu wa nchi hiyo na Somalia juu ya mpaka wa baharini wa pande hizo mbili.
-
AU yaunga mkono kuundwa kikosi cha pamoja nchini Somalia
Oct 12, 2021 04:37Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika limetangaza kuunga mkono pendekezo la kuundwa kikosi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa nchini Somalia, kitakachochukua nafasi ya Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika nchini humo (Amisom), iwapo wazo hilo litapasishwa.