-
Kiongozi wa RSF yuko Addis Ababa baada ya kushindwa kukutana na Al-Burhan
Dec 28, 2023 22:59Kamanda wa wapiganaji wa Kikosi cha Msaada wa Haraka kinachopigana na jeshi la Sudan, Luteni Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, aliwasili katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, jana Alhamisi baada ya kutembelea Uganda na kukutana na Rais Yoweri Museveni.
-
"Save Sudan"... Kampeni kuu kwenye mitandao ya kijamii ikiangazia yanayojiri nchini humo
Dec 21, 2023 23:36Wanaharakati wa mitandao ya kijamii wameanzisha kampeni kubwa iliyopewa jina la Save Sudan inayoangazia na kumulika masaibu yanayowapata wananchi wa Sudan kutokana na mapigano yanayoendelea nchini humo na kupuuzwa na jamii ya kimataifa hasa vyombo vya habari ambavyo aghlabu vimeelekeza mazingatio yao huko Gaza na mauaji ya raia wa Palesrina yanayofanywa na Israel.
-
WFP yasimamisha usambazaji wa chakula Sudan, mapigano yaenea
Dec 21, 2023 07:53Mpango wa Chakula Dunia (WFP) umesimamisha kwa muda utoaji na usambazaji wa chakula katika baadhi ya maeneo katika jimbo la al-Jazira katikati ya Sudan, huku mapigano yakipanuka na kuenea pande za mashariki na kusini mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.
-
AU yataka pande hasimu Sudan zisitishe mapigano
Dec 19, 2023 23:34Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika ametoa mwito kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na Jeshi la Sudan kusitisha uhasama na mapigano mara moja, na kwenda kwenye meza ya mazungumzo kwa shabaha ya kurejesha utulivu, uthabiti na amani endelevu katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
-
Mapigano nchini Sudan yapanuka hadi Wad Madani, maelfu ya watu wahama makazi yao
Dec 17, 2023 07:51Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vinapigana na Jeshi la Sudan nje ya mji wa Wad Madani katika Jimbo la Al-Jazira (katikati mwa Sudan) na kwamba mapigano hayo yamelazimisha maelfu ya raia kukimbia makazi yao na kuelekea maeneo salama.
-
UN yaiondoea vikwazo vya silaha Somalia, yahitimisha shughuli zake za kisiasa nchini Sudan
Dec 02, 2023 02:29Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio la kuondoa vikwazo vya mwisho vya silaha dhidi ya serikali ya Somalia na vikosi vyake vya usalama, huku likihitimisha pia shughuli za ujumbe wake wa kisiasa katika nchi ya Sudan iliyokumbwa na vita.
-
UN yatoa indhari: Idadi ya wanaokimbilia Sudan Kusini kutoka Sudan imeongezeka
Nov 10, 2023 03:26Mashirika ya kibindamu ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini yametahadharisha kuhusu ongezeko kubwa la watu wanaorejea na wakimbizi wanaokimbia mzozo na kuelekea kaskazini nchini Sudan.
-
Familia za Wasudan zatafuta hifadhi Sudan Kusini
Oct 27, 2023 09:39Ripoti zinasema kuwa katika hali ya kusikitisha, familia zinazoepuka ghasia na machafuko nchini Sudan zinaendelea kuwasili katika maeneo ya mbali ya kaskazini mwa Sudan Kusini.
-
UNHCR: Watu elfu nne wameuliwa Darfur, Sudan, mali za raia zimeharibiwa
Oct 18, 2023 00:20Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema, watu wapatao 4,000 wameuawa huku mali za raia zikiharibiwa katika mapigano yanayoendelea huko jimboni Darfur nchini Sudan, mapigano ambayo yalianzia kwenye mji mkuu Khartoum miezi sita iliyopita na kusambaa hadi nje ya mji huo, kati ya Jeshi la Serikali (SAF) na wanamgambo wa Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF).
-
Salva Kiir kuwa mwenyeji wa viongozi wa Sudan kujadili amani
Oct 17, 2023 10:42Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir amesema karibuni hivi atakuwa mwenyeji wa mkutano utakaowaleta pamoja viongozi wa pande mbili zinazopigana nchini Sudan, yaani Jeshi la Taifa la Sudan (SAF) na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF)