-
UN: Zaidi ya raia 1,000 waliuawa katika shambulio la RSF Darfur
Dec 18, 2025 08:22Ripoti iliyotolewa Alkhamisi na Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema zaidi ya raia 1,000 waliuawa wakati kundi la waasi wa Sudan lilipotwaa udhibiti wa kambi ya wakimbizi wa ndani huko Darfur nchini Sudan mwezi Aprili mwaka huu.
-
Takriban raia 2,000 waukimbia mji wa Heglig, Sudan baada ya kudhibitiwa na kikosi cha RSF
Dec 16, 2025 23:19Duru za habari ndani ya Sudan jana ziliarifu kuwa takriban raia 2,000 wameyaacha makazi yao katika mji wa Heglig wa magharibi mwa Sudan huko Kordofan Magharibi baada ya safari ngumu ya siku tisa ya kuhama makazi yao kufuatia kutekwa mji huo nawanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF).
-
UN yalaani shambulio lililoua askari 6 wa kulinda amani Sudan
Dec 13, 2025 23:06Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ameeleza kusikitishwa na shambulio la ndege isiyo na rubani lililolenga kituo cha Umoja wa Mataifa nchini Sudan, na kuwaua askari sita wa kulinda amani wa umoja huo.
-
RSF yatuhumiwa kuhusika na mengi ya matukio 1,300 ya ukatili wa kingono katika vita vya Sudan
Dec 12, 2025 06:44Shirika moja la kutetea haki za wanawake limesema, limerekodi matukio yapatayo 1,300 ya vitendo vya ukatili wa kingono na kijinsia vilivyofanywa katika vita vya ndani nchini Sudan huku Kikosi cha Usaidizi wa Haraka (RSF) kikishutumiwa kuhusika na akthari ya vitendo hivyo.
-
Sudan Kusini yatuma wanajeshi kulinda eneo muhimu la mafuta la Heglig nchini Sudan
Dec 11, 2025 23:11Sudan Kusini imetuma wanajeshi wake katika nchi jirani ya Sudan kwa lengo kulinda kisima cha kimkakati cha mafuta cha Heglig karibu na mpaka. Haya yamebainishwa jana Alhamisi na Mkuu wa jeshi la nchi siku chache baada ya Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kulidhibiti eneo hilo.
-
ICC imemhukumu kiongozi wa Janjaweed wa Darfur kifungo cha miaka 20 jela
Dec 09, 2025 08:05Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) leo Jumanne wamemhukumu kiongozi wa wanamgambo wa Janjaweed katika jimbo la Darfur Sudan kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya kufanya ukatili katika jimbo la Darfur.
-
AU yalaani shambulio la RSF lililoua zaidi ya raia 100 katika mji wa Kalogi, kusini mwa Sudan
Dec 07, 2025 23:05Umoja wa Afrika, AU umelaani vikali mashambulizi ya ndege zisizo na rubani yaliyofanywa na Vikosi vya Usaidizi wa Haraka, RSF yaliyoua makumi ya watu wakiwemo watoto katika mji wa Kalogi kusini mwa Sudan.
-
Sudan yawatuhumu wanamgambo wa RSF kwa kuuwa raia 79 huko Kordofan Kusini
Dec 06, 2025 10:02Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imewatuhumu wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kuwa wameua raia 79 wakiwemo watoto 43 katika mauaji ya halaiki kwenye mji wa Kalogi katika jimbo la Kordofan Kusini.
-
UN: Kuna hatari ya kuzuka wimbi jipya la mashambulizi na janga la kibinadamu Kordofan, Sudan
Dec 04, 2025 23:27Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, ametoa indhari kuhusu hatari ya kuzuka wimbi jipya la ukatili katika eneo la Kordofan, Sudan, baada ya kushadidi mapigano kati ya Jeshi la Sudan (SAF), Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) na Kundi la Harakati ya Kaskazini ya Ukombozi wa Wananchi wa Sudan, (SPLM-N).
-
Madaktari Sudan watahadharisha kuhusu hatima ya watoto na wanawake waliokwama Kordofan magharibi
Dec 04, 2025 00:18Kundi la madaktari wa Sudan limesema kuwa lina wasiwasi mkubwa kuhusu hatima ya makumi ya watoto na wanawake katika mji wa Babnousa huko Kordofan Magharibi, baada ya mapigano kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF).