-
Kuendelea maandamano ya Wasudan mjini Khartoum
Nov 30, 2021 08:28Wananchi wa Sudan wanaendelea kufanya maandamano kulalamikia mapatano ya kisiasa yaliyofikiwa nchini humo pamoja na kutaka serikali ya kiraia iundwe haraka nchini.
-
Waziri Mkuu wa Sudan awatimua wakuu wa jeshi la Polisi
Nov 28, 2021 04:15Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok amewauzulu wakuu wa jeshi la Polisi baada ya watu zaidi ya 40 kuuawa katika ukandamizaji uliofanywa na jeshi hilo kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya mwezi uliopita yaliyopelekea Hamdok mwenyewe kuondolewa madarakani.
-
Askari wasiopungua sita wa Sudan wauawa katika mapigano ya mpakani na Ethiopia
Nov 28, 2021 00:05Jeshi la Sudan limesema, askari wake kadhaa wameuawa katika shambulio lililofanywa na vikosi vya jeshi la Ethiopia katika eneo la mpakani linalozozaniwa na nchi mbili.
-
Viongozi wa kisiasa waachiwa huru Sudan baada ya kufanya mgomo wa kususia kula
Nov 27, 2021 09:02Wizara ya habari ya Sudan imetangaza kuwa, maafisa kadhaa wa kisiasa wa nchi hiyo wameachiwa huru kutoka jela walizokuwa wakishikiliwa baada ya kufanya mgomo wa kususia kula.
-
Wasudan washinikiza wanajeshi warudi makambini, kuundwe serikali ya raia
Nov 25, 2021 23:18Wananchi wa Sudan wameendelea na maandamano yao wakishinikiza wanajeshi warudi makambini ili waruhusu kuundwa serikali ya kiraia na ya kidemokrasia nchini humo.
-
Kuendelea mgogoro huko Sudan
Nov 24, 2021 22:58Licha ya kufikiwa mapatano ya kisiasa kati ya Abdel Fattah al Burhan Kamanda Mkuu wa Jeshi la Sudan na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abdallah Hamdok na kisha Waziri Mkuu huyo kurejeshwa madarakani, baadhi ya vyama vya kisiasa na akthari ya raia wa nchi hiyo wamepinga mapatano hayo na kumtuhumu Hamdok kuwa amewasaliti.
-
Jumuiya ya Nchi za Kiarabu yaunga mkono mwafaka wa kisiasa uliofikiwa nchini Sudan
Nov 24, 2021 12:49Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amesema, jumuiya hiyo inaunga mkono makubaliano ya kisiasa yaliyofikiwa nchini Sudan.
-
Mwanadiplomasia wa zamani: Israel na Misri ziliunga mapinduzi ya kijeshi Sudan
Nov 24, 2021 04:03Waziri wa Mambo ya Nje wa Zamani wa Sudan amesema kuwa, Misri na utawala wa Kizayuni wa Israel ziliunga mkono mapinduzi ya kijeshi nchini mwake.
-
AU yapongeza kufikiwa makubaliano ya kisiasa Sudan, maandamano yaendelea
Nov 22, 2021 08:42Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika amepongeza hatua ya kufikiwa makubaliano mapya ya kisiasa nchini Sudan akisisitiza kuwa, mapatano hayo ni hatua moja mbele ya kurejesha utawala wa Katiba nchini humo.
-
Mapatano ya kisiasa Sudan; kuendelea mgogoro
Nov 22, 2021 07:50Kufuatia kuendelea maandamano na malalamiko ya watu wa Sudan, hatimaye majenerali wanaotawala nchi hiyo wamefikia mapatano na Waziri Mkuu Abdalla Hamdok kwa ajili ya kutatua mgogoro unaoikabili nchi hiyo. Kwa msingi huo Hamdok tokea Jumatatu anaendelea kuhudumu kama waziri mkuu wa Sudan.