-
Washiriki wa Mkutano wa Usalama Tehran: Uingiliaji wa madola ya kigeni, chanzo cha ukosefu wa amani
Jan 09, 2018 04:40Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Usalama Tehran umemalizika kwa washiriki kusisitiza kuwa, uingiliaji wa madola makubwa ya kigeni yaliyo nje ya eneo la Asia Magharibi ndio chanzo kikuu cha ukosefu wa usalama na uthabiti katika eneo hili.
-
Zarif: Uchochezi wa kikaumu nchini Syria na Iraq ni hatari kwa eneo na dunia nzima
Jan 08, 2018 16:30Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, ni jambo la dharura kulindwa umoja na mshikamano wa kitaifa na ardhi nzima za eneo hili na kusisitiza kuwa, chokochoko na uchochezi wa kikaumu na kikabila pamoja na fikra za kujitenga katika nchi za Iraq na Syria ni hatari kwa eneo hili na dunia nzima.
-
Kuanza Mkutano wa Pili wa Usalama wa Tehran kwa kuhudhuriwa na viongozi kutoka nchi 49 duniani
Jan 08, 2018 08:11Mji mkuu wa Iran, Tehran leo Jumatatu utakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Usalama katika eneo la Magharibi mwa Asia unaojulikana kama "Mkutano wa Usalama wa Tehran" kufuatia changamoto mbalimbali zinazolikabili eneo hili la kistratejia.
-
Tehran mwenyeji wa Kongamano la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu
Dec 05, 2017 08:08Duru ya 31 ya Kongamano la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu imeng'oa nanga hii leo hapa katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Tehran.
-
Mkutano wa Kimataifa wa Wapenzi wa Ahlul-Baiti AS umeanza leo hapa mjini Tehran + SAUTI
Nov 22, 2017 12:12Mkutano wa Kimataifa wa Wapenzi wa Ahlul-Baiti (as) umeanza leo hapa mjini Tehran kwa kuhudhuriwa na shakhsia, wanazuoni na wanafikra 500 kutoka katika ulimwengu wa Kiislamu.
-
Iran yasisitiza haingilii mambo ya ndani ya nchi nyingine
Nov 13, 2017 15:34Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: "Sera ya kimsingi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kutoingilia kamwe masuala ya ndani ya nchi nyingine."
-
Qassemi: Viongozi wa Saudi Arabia wanafanya njama za kuanzisha adui bandia
Oct 30, 2017 13:53Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kujadiliwa masuala ya pande mbili, kieneo, kimataifa, vita dhidi ya ugaidi na kupanua ushirikiano wa pande mbili ndizo ajenda kuu za kikao cha pande tatu cha viongozi wa Iran, Russia na Azerbaijan.
-
Kikao cha Umoja wa Mabunge ya OIC kufanyika kesho Tehran
Oct 06, 2017 08:14Kikao cha 38 cha Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (PUIC) kitafanyika kesho Jumamosi kwenye makao makuu ya umoja huo hapa Tehran.
-
Wanachuo waandamana Tehran kuunga mkono Waislamu wa Myanmar
Sep 11, 2017 03:18Wanafunzi mbalimbali wa vyuo vikuu nchini Iran wamefanya maandamano mbele ya ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Tehran na kuzitaka nchi za Kiislamu na jamii ya kimataifa hasa hasa Umoja wa Mataifa kutoendelea kunyamazia kimya mauaji ya kimbari wanayofanyiwa Waislamu wa Myanmar.
-
Spika wa Bunge la Afrika Kusini awasili Iran
Sep 01, 2017 15:17Spika wa Bunge la Afrika Kusini amewasili Tehran kwa ajili ya kufanya mazungumzo na maafisa wa ngazi za juu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.