-
Viongozi wa Ufaransa waendelea kutoa madai ya chuki dhidi ya Uislamu
Nov 26, 2020 23:00Huku hasira za Waislamu kwa vitendo na matamshi ya chuki dhidi ya Uislamu nchini Ufaransa zikawa bado hazijapoa, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi hiyo ya bara Ulaya Jean-Yves Le Drian amejitokeza na kudai kwamba, baadhi ya mataifa yanataka kuwadhibiti Waislamu wa Ufaransa.
-
Ufaransa yashiriki kwa kiwango kikubwa kuangamiza raia nchini Yemen
Nov 23, 2020 22:53Vyombo vya habari vya Ufaransa vimefichua kuwa, serikali ya nchi hiyo inashiriki vilivyo katika kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Saudi Arabia na kuwaua kwa umati wananchi wa Yemen.
-
Kuendelea chuki za rais wa Ufaransa dhidi ya Uislamu
Nov 22, 2020 21:34Ikiwa ni kuendeleza chuki zake dhidi ya Uislamu na Waislamu, rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, sasa ametoa muhula maalumu kwa viongozi wa makundi ya Kiislamu ya nchi hiyo kuhakikisha wanajivika utamaduni wa Magharibi hata katika mambo ambayo ni haramu kwa mujibu wa mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu.
-
Wapakistan: Hatutositisha maandamano mpaka balozi wa Ufaransa atimuliwe
Nov 16, 2020 03:41Maelfu ya waandamanaji nchini Pakistan waliofanya mgomo wa kuketi wametangaza kuwa wataendeleza mgomo wao huo mpaka balozi wa Ufaransa nchini humo atimuliwe.
-
Kukosolewa vikali madai ya kuwepo uhuru wa kujieleza nchini Ufaransa
Nov 15, 2020 23:03Mwenendo wa chuki na kukejeliwa itikadi za Waislamu nchini Ufaransa umeshika kasi katika miaka ya karibuni, na katika uwanja huo kuchapishwa tena na jarida la Charlie Hebdo, vikatuni vinamvyodhalilisha Mtume Mtukufu wa Uislamu (saw) kumewakasirisha sana Waislamu.
-
Amnesty: Kwa undumakuwili ilionao, Ufaransa haiwezi kudai inaunga mkono uhuru wa kutoa maoni
Nov 15, 2020 00:32Shirika la Msamaha Duniani, Amnesty International limekosoa mtazamo wa kiundumakuwili wa serikali ya Ufaransa na kusisitiza kuwa, serikali hiyo haiwezi kudai kwamba inaunga mkono uhuru wa kutoa maoni.
-
Kiongozi wa ngazi za juu wa al-Qaeda auawa kaskazini mwa Mali
Nov 14, 2020 04:06Kiongozi wa operesheni za kijeshi wa tawi la kundi la al-Qaida kanda ya Afrika Kaskazini ameuawa katika operesheni ya jeshi la Ufaransa nchini Mali.
-
Kansela wa Ujerumani akwepa kulaani vitendo vya kuvunjia heshima matukufu ya Uislamu
Nov 11, 2020 11:13Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amekwepa kulaani hatua na vitendo vya kuvunjia heshima thamani na matukufu ya Uislamu.
-
Juhudi za Ufaransa za kujaribu kupunguza hasira ya Waislamu duniani
Nov 09, 2020 23:09Uadui wa viongozi wa Ufaransa dhidi ya Uislamu, umeamsha hasira ya Waislamu katika pembe zote za dunia kadiri kwamba nchi nyingi za Kiislamu zimelaani msimamo huo wa Wafaransa, bali zimeanzisha harakati za kususia bidhaa zinazotengenezwa Ufaransa ili kuonyesha kuchukizwa kwao na uadui huo wa viongozi wa Paris.
-
Vijana Waislamu wa Ufaransa wajitolea kulinda makanisa ya nchi hiyo
Nov 07, 2020 23:07Licha ya hatua na matamshi ya kiuadui na ya chuki yaliyotolewa na viongozi wa Ufaransa dhidi ya Uislamu, kundi moja la vijana Waislamu Wafaransa wamejitolea kulinda usalama wa makanisa ya nchi hiyo.